Towashi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Towashi mkuu wa ikulu ya Sultani wa Uturuki aliyekabidhiwa wake zake.

Towashi (kutoka neno la Kiajemi) ni mwanamume asiyeweza tendo la ndoa, kwa mfano yule aliyehasiwa.

Katika historia ilitokea mara nyingi na kwa sababu mbalimbali kwamba watu wa namna hiyo walihitajiwa, kwa mfano ili kutunza wake wa mfalme, kufanya kazi kama mtumwa bila kuzaa watoto, kubaki na sauti ndogo ya kabla ya ubalehe ili kuimba vizuri, n.k.

Siku hizi watu wanakubaliana katika kulaani upasuaji kama huo kwa kuwa ni kinyume cha hadhi ya binadamu ambaye ni haki yake ya msingi kuwa na mwili mtimilifu na kutofanywa chombo cha wengine.

Katika Injili (Math 19:12), Yesu alifananisha watu ambao kama yeye kwa ajili ya ufalme wa Mungu wanajinyima kwa hiari ndoa na uzazi na matowashi waliozaliwa na ubovu katika viungo vya uzazi na wale waliohasiwa. Sababu ni kwamba uamuzi wao wa moja kwa moja unawanyima tunu hizo, hivyo ni sadaka ambayo wanamtolea Mungu ili kueneza zaidi utawala wake.

Ingawa katika Agano la Kale matowashi hawakuruhusiwa kujiunga na dini ya Israeli, Isaya wa Tatu alitabiri kwamba siku za mbele hali yao itakuwa tofauti.

Hivyo katika Matendo ya Mitume (sura ya 8) inasimuliwa jinsi Towashi Mwethiopia alivyobatizwa na Filipo mwinjilisti.

Nukuu kutoka katika Mathayo 19:12

"Maana wako matowashi waliozaliwa hali hiyo toka matumboni mwa mama zao; tena wako matowashi waliofanywa na watu kuwa matowashi; tena wako matowashi waliojifanya kuwa matowashi kwa ajili ya ufalme wa mbinguni. Awezaye kulipokea neno hili, na alipokee." Mathayo 19:12 SUV

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Makala hii kuhusu mambo ya biolojia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Towashi kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.