Nenda kwa yaliyomo

Towashi Mwethiopia

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rembrandt, Ubatizo wa Towashi, 1626 hivi.

Towashi Mwethiopia ni mtu wa Agano Jipya katika Biblia aliyeingizwa na Filipo mwinjilisti katika Ukristo.

Kabla yake alikuwa amevutiwa sana na dini ya Uyahudi lakini hakuweza kupokewa kwa sababu ya ubovu wake kijinsia (Kumb 23:1).

Habari za wongofu na ubatizo zinasimuliwa katika kitabu cha Matendo ya Mitume sura ya 8 na zinalenga kuonyesha jinsi Injili ya Yesu Kristo ilivyozidi kuenea hata kwa mataifa ya mbali sana.

Ni Mwafrika wa kwanza kutoka kusini kwa Sahara kujulikana kama Mkristo.

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.