Jeshi la Ardhi la Kenya

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search

Jeshi la Ardhi la Kenya ni tawi la wanajeshi wa ardhini la Majeshi ya Ulinzi ya Kenya

Historia[hariri | hariri chanzo]

Jeshi la leo lilitokana na King's African Rifles.[1] 

Mwezi Agosti 1895, serikali ya Uingereza ilikubali kuanzishwa kwa kikosi kilichojumuisha Wapunjabi 300, Waswahili 300, Wasudani 100 na wanajeshi 200 kutoka makabila mbalimbali katika kanda. Kikosi hicho kiliitwa East African Rifles na kilikuwa kimetengenezwa kutoka kikosi cha awali, IBEA katika Mombasa (Fort Jesus).

King's African Rifles walipigana dhidi ya Mau Mau chini ya amri ya maafisa wa Uingereza na upande Wakenya waaminifu kwa wakoloni na wale ambao walitetea amani ili kupata uhuru, kama vile Jomo Kenyatta.

Misheni za ulinzi amani na migogoro mingineyo[hariri | hariri chanzo]

Mbali na jukumu la msingi la ulinzi wa Jamhuri ya Kenya na jukumu la misaada kwa mashirika ya mamlaka, Jeshi la Kenya hushiriki katika shughuli za kudumisha amani ya kimataifa. Jeshi la Kenya lilijihusisha na shughuli za misaada ya amani mwaka 1973 lilipokubali ombi la Umoja wa Mataifa kwa Jamuhuri ya Kenya kutoa vikosi baada ya vita vya Waarabu na Waisraeli. Hata hivyo, jeshi halikuweza kujifikisha kwa sababu ya matatizo katika uhamishaji.

Mara ya kwanza ya Jeshi la Kenya kushiriki kikamilifu katika kudumisha amani ilikuwa mwaka 1979, wakati Jumuiya ya Madola iliomba Jamhuri ya Kenya kuchangia wanajeshi ili kudumisha amani katika Rhodesia ya Kusini (sasa Zimbabwe). Nchi ilikuwa inakabiliwa na vita vya ukombozi.

Tangu mwaka 1989, Kenya imechangia waangalizi wa kijeshi, wafanyakazi, polisi wasimamizi wa raia na wanajeshi wa miguu.[2] Kiwango cha ushiriki huo umejumuisha makamanda wa vikosi, mwangalizi mkuu wa jeshi, Majenerali wakuu katika misheni zifuatazo za UM na UA:

Kwa sasa, walinzi amani wa Umoja wa Mataifa kutoka Kenya wametumika katika nchi 16 tofauti katika Afrika, Mashariki ya Kati, Balkani na Asia. 

Miundo na huduma[hariri | hariri chanzo]

Miundo ya Jeshi la Kenya[hariri | hariri chanzo]

 • Wanajeshi wa Miguu wa Jeshi la Kenya
 • Wanajeshi wa Kuruka wa Jeshi la Kenya
 • Hifadhi ya Ala za Jeshi la Kenya (hujumuisha Batalioni 78 ya Vifaru, Isiolo)
 • Vifyatuzi vya Jeshi la Kenya (hujumuisha Batalioni 78 ya Vifyatuzi)
 • Wahandisi wa Jeshi la Kenya
 • Batalioni ya Farasi na Hewani ya 50

Huduma za Jeshi la Kenya[hariri | hariri chanzo]

 • Wanajeshi Wahamishaji vifaa wa Jeshi la Kenya
 • Wanajeshi Wasafirishaji wa Jeshi la Kenya
 • Uhandisi Mitambo na Umeme
 • Kenya Corps Jeshi ya Ishara
 • Jeshi La Polisi
 • Jeshi la Elimu
 • Batalioni ya Matibaby
 • Makonstebo wa Jeshi

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

 1. Ministry of Defence – Kenya. Iliwekwa mnamo 13 August 2017.
 2. Peacekeeping Operations. Jalada kutoka ya awali juu ya 2013-09-27. Iliwekwa mnamo 2013-04-25.