Elzeari wa Sabran

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Masalia ya Mt. Elzeari na mwenye heri Delfina katika kanisa la Kifransisko la Ansouis, Ufaransa.

Elzeari wa Sabran, T.O.S.F., mtawala wa Ansouis na Ariano, alizaliwa katika ngome ya Saint-Jean-de-Robians, karibu na Cabrières-d'Aigues, Provence, Ufaransa Kusini, mwaka 1285. Alifariki Paris, tarehe 27 Septemba 1323.

Maisha[hariri | hariri chanzo]

Ujanani Elzéar alipewa malezi bora ya Kikristo na katika sayansi chini ya usimamizi wa abati William wa Sabran, ndugu ya baba yake, kwenye Abasia ya Mt. Viktori, huko Marseille.

Alipofikia umri wa kuoa, alikubali pendekezo la mfalme Charles II wa Napoli akamuoa Delfina wa Glandèves (12841358).

Usiku wa kwanza baada ya arusi, Delfina alimuarifu kuwa aliweka nadhiri ya useja. Ingawa sheria za Kanisa zilikuwa zinampa mume haki ya kumdai asifuate nadhiri hiyo, Elzéar aliamua kuiheshimu na kukubali mwenyewe pia kuweka nadhiri kama hiyo na kuishi naye kama kaka na dada.

Hapo walijiunga na Utawa wa Tatu wa Mt. Fransisko.

Elzéar na Delfina waliishi kwa sala, malipizi na matendo ya huruma kwa maskini.

Alipofikia umri wa miaka 20, walihamia Puimichel ili kufaidika na upweke mkubwa zaidi, na aliwapangia watumishi wake taratibu zilizofanya nyumba yake kielelezo cha maadili ya Kikristo.

Baba yake alipofariki mwaka 1309, alikwenda kutamalaki maeneo yake mapya nchini Italia. Huko wema wake ulimvutia heshima na uaminifu wa wenyeji waliokuwa wamedharau kwanza watawala wao wa kabila la Wanormani.

Mwaka 1312 alielekea Roma kama kiongozi wa jeshi la mfalme Roberto wa Napoli ili kusaidia kumfukuza Kaisari Henry VII kutoka mji huo wa Papa.

Baada ya vita alirudi Provence, alipoanzisha tena nyumba ulimofuatwa uadilifu wa hali ya juu.

Mwaka 1317 Elzéar alikwenda Napoli awe mlezi wa Charles wa Calabria, mtoto wa mfalme Roberto. Akazidi kumsaidia huyo mtoto alipopata kuwa makamu wa baba yake katika Ufalme wa Sicilia.

Mwaka 1323 alitumwa kama balozi kwa mfalme wa Ufaransa ili kumuomba binti yake Maria wa Valois (1309-1332) aolewe na Charles. Kwenye ikulu alijenga wote kwa maadili yake ya kishujaa. Kisha kufanikisha mpango huo alifariki hukohuko.

Heshima baada ya kifo[hariri | hariri chanzo]

Alitangazwa mtakatifu kwa hati ya Papa Urban V (ambaye Elzeari alikuwa amemsimamia kwenye sakramenti), na kwa utekelezaji wa Papa Gregori XI mwaka 1371 hivi.

Wakati huohuo mke wake Delfina alitangazwa na papa Urban V kuwa mwenye heri.

Sikukuu yao ya pamoja inaadhimishwa tarehe 26 Septemba.

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

Christian cross.svg Makala hii kuhusu Mkristo huyu bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Elzeari wa Sabran kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.