Abasia

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Abasia ya Monte Cassino iliyoanzishwa na Benedikto wa Nursia

Abasia ni aina ya monasteri katika Kanisa Katoliki ambayo inaongozwa na abati au abesi na inajitegemea kufuatana na Sheria za Kanisa.

Abasia inaweza kuwa na monasteri ndogo chini yake zinazoongozwa na priori aliye chini ya usimamizi wa abati.