Sierra Leone
| |||||
Kaulimbiu ya taifa: Unity - Freedom - Justice (Umoja, Uhuru, Haki) | |||||
Wimbo wa taifa: High We Exalt Thee, Realm of the Free (Twakusifu nchi ya watu huru) | |||||
Mji mkuu | Freetown | ||||
Mji mkubwa nchini | Freetown | ||||
Lugha rasmi | Kiingereza | ||||
Serikali | Jamhuri Julius Maada Bio | ||||
Uhuru kutoka Uingereza |
27 Aprili 1961 | ||||
Eneo - Jumla - Maji (%) |
71,740 km² (ya 119) 1.1 | ||||
Idadi ya watu - Julai 2023 kadirio - 2000 sensa - Msongamano wa watu |
8,909,040 (ya 100 1) 5,426,618 112/km² (ya 114 1) | ||||
Fedha | Leone (SLL )
| ||||
Saa za eneo - Kiangazi (DST) |
GMT (UTC+0) (UTC) | ||||
Intaneti TLD | .sl | ||||
Kodi ya simu | +232
- |
Sierra Leone ni nchi ya Afrika ya Magharibi.
Imepakana na Guinea na Liberia, upande wa magharibi iko bahari ya Atlantiki.
Jina la nchi lina asili ya Kireno na linamaanisha "Mlima wa Simba".
Ni koloni la zamani la Uingereza na tangu 27 Aprili 1961 ni jamhuri huru.
Sierra Leone ni kati ya nchi maskini sana duniani.
Historia
[hariri | hariri chanzo]Nchi yenyewe ilianzishwa na Waingereza kwa kuunda mji wa Freetown ("Mji wa watu huru") mwaka 1787[1]. Kusudi lake likuwa kuwarudisha Afrika watu waliowahi kuwa watumwa. Kiasili wale wakazi wa kwanza walikuwa watumwa weusi waliopewa uhuru kwa sababu walishikamana na Waingereza dhidi ya Wamarekani katika vita vya uhuru wa Marekani.
Baadaye Waingereza wapinzani wa utumwa walinunua watumwa wakiwapa uhuru na kuwapeleka Sierra Leone.
Tangu mwaka 1807 Uingereza ulikataza biashara ya watumwa (lakini utumwa wenyewe bado) na watumwa waliopatikana kwenye meli za biashara hiyo haramu walipelekwa Sierra Leone na kupewa uhuru.
Ikianzishwa na shirika la wapinzani wa utumwa Sierra Leone ikajwa koloni la kwanza la Uingereza katika Afrika ya Magharibi mwaka 1792. Kuanzia mwaka 1802 Freetown ilikuwa makao makuu ya Kiingereza kwa Afrika ya Magharibi.
Mwaka 1961 Sierra Leone ilipewa uhuru wake.
Miaka 1994 - 2002 nchi ilikuwa na vita vya wenyewe kwa wenyewe. Tangu mwisho wake nchi inajengwa tena.
Watu
[hariri | hariri chanzo]Wakazi asili wamegawanyika katika makabila 16, kila moja likiwa na lugha na utamaduni maalumu; kati yake makubwa zaidi ni Watemmne (35.5%) na Watembe (33.2%).
Lugha inayojulikana na asilimia 96 za wakazi ni Kikrio, aina ya Krioli ya Kiingereza iliyochanganya pia lugha mbalibali za Kiafrika. Lakini lugha rasmi ni Kiingereza.
Upande wa dini, Waislamu ni 78.5%, Wakristo ni 20.4% na wafuasi wa dini asilia za Kiafrika hawafikii 2%. Sierra Leone ni nchi isiyo na dini rasmi.
Tazama pia
[hariri | hariri chanzo]- Orodha ya lugha za Sierra Leone
- Orodha ya nchi kufuatana na wakazi
- Orodha ya nchi za Afrika kulingana na idadi ya watu
- Orodha ya nchi za Afrika kulingana na msongamano wa watu
- Orodha ya nchi za Afrika kulingana na pato la taifa
- Demografia ya Afrika
Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]- ↑ "Sierra Leone | Culture, History, & People | Britannica". www.britannica.com (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2023-02-26.
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- Acemoglu, Daron, Tristan Reed, and James A. Robinson. "Chiefs: Economic Development and Elite Control of Civil Society in Sierra Leone," Journal of Political Economy (2014) 122#2 pp. 319–368 in JSTOR
- Imodale Caulker-Burnett, The Caulkers of Sierra Leone: The Story of a Ruling Family and Their Times (Xlibris, 2010)
- Harris, David. Civil War and Democracy in West Africa: Conflict Resolution, Elections and Justice in Sierra Leone and Liberia, I.B. Tauris, 2012
- Keen, David (2005). Conflict and Collusion in Sierra Leone. Oxford: James Currey. ISBN 0-85255-883-X.
- Kup, Alexander Peter (1961). A History of Sierra Leone, 1400–1787. Cambridge: Cambridge University Press. ISBN 0-7864-1814-1.
- Sillinger, Brett (2003). Sierra Leone: Current Issues and Background. New York: Nova Science Publishers. ISBN 1-59033-662-3.
- Utting, Francis A (1931). The Story of Sierra Leone. Ayer Company Publishers. ISBN 0-8369-6704-6.
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- Serikali
- The Republic of Sierra Leone official government site
- Chief of State and Cabinet Members Ilihifadhiwa 5 Septemba 2015 kwenye Wayback Machine.
- Ministry of Mineral Resources official government minerals site
- thepatrioticvanguard.com The Patriotic Vanguard – official government newspaper
- Taarifa za jumla
- Country Profile, BBC News
- Sierra Leone entry at The World Factbook
- Sierra Leone Ilihifadhiwa 7 Juni 2008 kwenye Wayback Machine., UCB Libraries GovPubs
- Sierra Leone katika Open Directory Project
- Wikimedia Atlas of Sierra Leone
- Key Development Forecasts for Sierra Leone, International Futures
- Vyombo vya habari
- Awareness Times Ilihifadhiwa 5 Septemba 2008 kwenye Wayback Machine. Newspaper
- The New People, nNewspaper
- News headline links, AllAfrica.com
- Sierra Leone News & Blog Ilihifadhiwa 19 Septemba 2015 kwenye Wayback Machine., Current Sierra Leone News & Blog
- Trade
- Tourism
- National Tourist Board of Sierra Leone Ilihifadhiwa 14 Januari 2010 kwenye Wayback Machine. official site
- Mengineyo
- Sierra Leone Forum Ilihifadhiwa 6 Septemba 2015 kwenye Wayback Machine.
- Friends of Sierra Leone
- Schools for Salone, non-profit dedicated to rebuilding schools
- ENCISS civil society and governance
- The Auradicals Club Ilihifadhiwa 10 Mei 2011 kwenye Wayback Machine., Student Club in Fourah Bay College
- Sierra Leone Web
- Sweet Salone, 2008 film on new music in Sierra Leone
- War Crimes Trials in Sierra Leone
- Hurrarc – Human Rights Respect Awareness Raising Campaigners Ilihifadhiwa 14 Julai 2014 kwenye Wayback Machine., Sierra Leone NGO
- Stories from Lakka Beach Ilihifadhiwa 29 Juni 2014 kwenye Wayback Machine., 2011 documentary about life in a post-conflict beach town
Nchi za Afrika | |
---|---|
Afrika ya Kati (Jamhuri ya) | Afrika Kusini | Algeria | Angola | Benin | Botswana | Burkina Faso | Burundi | Cabo Verde | Chad | Cote d'Ivoire | Eritrea | Eswatini | Ethiopia | Gabon | Gambia | Ghana | Guinea | Guinea Bisau | Guinea ya Ikweta | Jibuti | Kamerun | Kenya | Komori | Kongo (Jamhuri ya) | Kongo (Jamhuri ya Kidemokrasia ya) | Lesotho | Liberia | Libya | Madagaska | Malawi | Mali | Misri | Morisi (Visiwa vya) | Mauritania | Moroko | Msumbiji | Namibia | Niger | Nigeria | Rwanda | Sahara ya Magharibi | Sao Tome na Principe | Senegal | Shelisheli | Sierra Leone | Somalia | Sudan | Sudan Kusini | Tanzania | Togo | Tunisia | Uganda | Zambia | Zimbabwe | |
Maeneo ya Afrika ambayo ni sehemu za nchi nje ya Afrika | |
Hispania: Kanari · Ceuta · Melilla | Italia: Pantelleria · Pelagie | Ufaransa: Mayotte · Réunion | Uingereza: · St. Helena · Diego Garcia | Ureno: Madeira |
Makala hii kuhusu maeneo ya Afrika bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Sierra Leone kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |