Freetown

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Muonekano wa Mji wa Freetown


Jiji la Freetown
Nchi Sierra Leone

Freetown ni mji mkuu pamoja na badari kubwa na kitovu cha uchumi wa nchi Sierra Leone. Iko kwenye kando la Atlantiki kwenye rasi ya Freetown. Idadi ya wakazi ni 1,070,000.

Mji uliundwa 1787 kwa ajili ya watumwa wenye asili ya Afrika waliowekwa huru. Hapo ni asili ya jina "Freetown" linalomaanisha "Mji wa watu huru".

Ulikuwa mji mkuu wa koloni za Uingereza katika Afrika ya Magharibi kati ya 1808 hadi 1874.

Hadi leo Makreoli ambao ni watoto wa watumwa waliopewa uhuru kama walowezi ni tabaka la pekee Freetown wakionekana kwa utamaduni na lugha ya pekee.

Katika miaka ya 1990 mji ulikuwa mahali pa mapigano kati ya wanamgambo na askari za ECOWAS.

Uchumi[hariri | hariri chanzo]

Uchumi wa Freetown unategemea hasa bandari. Kuna pia viwanda vya sigara, vya kutengeneza petroli, vya chakula na za kusafisha almasi.