Lango:Afrika

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Milango ya Wikipedia: Sanaa · Utamaduni · Jiografia · Afya · Historia · Hisabati · Sayansi · Falsafa · Dini · Jamii · Teknolojia

hariri  fuatilia  

Lango la Afrika

Afrika ni bara la pili duniani kwa ukubwa, likiwa na eneo la kilometa za mraba zipatazo 30,370,000 na kwa idadi ya wakazi, hao wakiwa 1,225,080,510 (mwaka 2016). Asia ndiyo bara pekee la kushinda Afrika.

Neno "Afrika" limetokana na lugha ya Kilatini ya Roma ya Kale. Waroma kwa jina hilo hawakumaanisha bara lote bali eneo katika Tunisia ya leo tu. Asili yake ni kabila la "Afrig" lililoishi sehemu zile. Wakati huo Wagiriki wa Kale walitumia zaidi jina la Libya kwa ajili ya nchi kusini kwa Bahari ya Mediteraneo. Maeneo ya ndani kuelekea kusini mara nyingi yaliitwa kwa jina la "Ethiopia" linalomaanisha nchi ya watu weusiweusi (kwa Kigiriki "aithiops": aliyechomwa na jua).

hariri  fuatilia  

Nchi za Afrika

hariri  fuatilia  

Jamii

hariri  fuatilia  

Wasifu Uliochaguliwa

Picha ya Shaka Zulu mnamo mwaka 1824

Shaka (pia: Tshaka, Tchaka au Chaka; halafu: Shaka Zulu, Shaka ka Senzangakhona) (* takriban 1781 - 1828 BK) alikuwa kiongozi wa Wazulu aliyebadilisha ukoo mdogo wa Kinguni kuwa kabila au taifa kubwa lililotawala maeneo mapana ya Afrika Kusini hasa Natal ya leo. Sifa zake zimetokana na uwezo wa kupanusha utawala wake kutoka eneo ndogo la 260 km² kuwa 28.500 km², kuvunja nguvu ya makabila mengine na kuyaunganisha na taifa lake. Katika historia ya kijeshi ya Afrika alianzisha mbinu mpya zilizopanusha uwezo na enzi yake.


hariri  fuatilia  

Makala iliyochaguliwa

Eneo la Zanj ya kihistoria kwenye ramani ya Afrika ya Mashariki
Zanj (Kiarabu na Kifarsi زنج) ni neno lililotumiwa na waandishi Waislamu wa zamani kutaja watu weusi kutoka Afrika ya Mashariki na pia kwa maana ya kijiografia kutaja eneo la Afrika ya Mashariki. Wanajiografia Waislamu walihesabu pwani takriban kati ya Mogadishu na kisiwa cha Pemba kuwa "Zanj". Kusini yake waliita nchji ya Sofala na kaskazini yake nchi ya Berbera kufuatana na mabandari ya nyakati ziule zilizojulikana kwao. Uwezekano mkubwa ni neno hili Zanj latokana na jina la kijiografia la awali "Azania" likatumiwa baadaye kutaja hasa kisiwa cha Zanzibar. Baadaye Zanj imejulikana kama nchi ya Waswahili. Waandishi Waarabu wa kale waliita hasa watu weusi kutoka Afrika ya Mashariki kwa jina hili la "Zanj". Waliwatofautiana na Waafrika weusi wengine kama Wanubia (taz. Nubia) au Wahabash (taz. Uhabeshi). Walitazamiwa kuwa watu wenye hali na maendeleo ya duni kulingana na wenyeji wengine wa Afrika iliyojulikana kwa Waarabu.


hariri  fuatilia  

Picha Iliyochaguliwa


Murchison Falls kutoka juu, Uganda
(kupata bango)


hariri  fuatilia  

Je, wajua...?

...kwamba Kisiwa cha Saanane ni hifadhi tarajiwa ambayo ina eneo la mita 0.5, na iko umbali wa kilometa 2 kusini magharibi kutoka katikati ya jiji la Mwanza, katika Ghuba ya Ziwa Victoria nchini Tanzania.

hariri  fuatilia  

Masharika ya Wikimedia