Lango:Afrika/Wasifu uliochaguliwa

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Wasifu Uliochaguliwa[hariri chanzo]

Wasifu Uliochaguliwa kwa Mei 2012[hariri chanzo]

Picha ya Shaka Zulu mnamo mwaka 1824

Shaka (pia: Tshaka, Tchaka au Chaka; halafu: Shaka Zulu, Shaka ka Senzangakhona) (* takriban 1781 - 1828 BK) alikuwa kiongozi wa Wazulu aliyebadilisha ukoo mdogo wa Kinguni kuwa kabila au taifa kubwa lililotawala maeneo mapana ya Afrika Kusini hasa Natal ya leo. Sifa zake zimetokana na uwezo wa kupanusha utawala wake kutoka eneo ndogo la 260 km² kuwa 28.500 km², kuvunja nguvu ya makabila mengine na kuyaunganisha na taifa lake. Katika historia ya kijeshi ya Afrika alianzisha mbinu mpya zilizopanusha uwezo na enzi yake.