Kofi Annan

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Kofi Annan

Kofi Annan alikuwa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa 1996 - 2006. Alizaliwa 8 Aprili 1938 huko Kumasi, Ghana. Alipewa jina Kofi kuonyesha kuwa alizaliwa siku ya Ijumaa kuendana na utamaduni wa Ashanti. Jina Annan linamaanisha kuwa alikuwa ni mtoto wa nne kuzaliwa.

Yaliyomo

[hariri] Mtumishi wa Umoja wa Mataifa

Baada ya masomo ya uchumi alijiunga na huduma ya Umoja wa Mataifa mwaka 1962 katika WHO. 1974-1976 alifanya kazi Ghana halafu akarudi tena huduma ya UM. Akapanda ngazi kuwa Makamu wa Katibu Mkuu mhusika wa usalama aliwajibika kusimamia shughuli za wanajeshi walio chini ya UM.

Alihusika na vita ya Rwanda pia ya Yugoslavia ambako wanajeshi chini ya bendera ya UM walishirikiana.

[hariri] Katibu Mkuu

1996 alichaguliwa kuwa Katibu Mkuu wa UM, akarudishwa cheo mwaka 2001. Tangu 1 Januari alifuatwa ofisini na Ban Ki-moon.

[hariri] Mpatanishi nchini Kenya

Mwaka 2008 Annan alirudi katika habari za kimataifa alipofika Kenya kwa shabaha ya kupatanisha viongozi wa kisiasa waliopigana juu ya matokeo ya uchaguzi wa rais wa Kenya 2007. Akisaidiana na Grace Machel na rais mstaafu wa Tanzania Benjamin Mkapa aliendesha majadiliano kati ya wawakilishi wa ODM na PNU kwa muda wa wiki 5. Akafaulu kuleta mapatano ya ushirikiano kati ya pande zote mbili.

[hariri] Maisha ya binafsi

Kofi Annan ameoa mara ya pili. Mke wake Nane Maria Annan anatoka Uswidi. Ana watoto watatu.

Vifaa binafsi
Maeneo ya wiki

Vibadala
Vitendo
Urambazaji
Vifaa
Lugha zingine