Lango:Afrika/Makala iliyochaguliwa
Makala iliyochaguliwa[hariri chanzo]
- 01 Januari 2012 : Nembo ya Uganda
- 01 Februari 2012 : Chuo Kikuu cha Cape Town
- 01 Machi 2012 : Eratosthenes
- 01 Aprili 2012 : Kampeni za Kivita katika Afrika ya Mashariki (Vita ya Kwanza ya Dunia)
- 01 Mei 2012 : Zanj
- 01 Juni 2012 : Jimbo Katoliki la Zanzibar
- 01 Julai 2012 : Assia Djebar
- 01 Agosti 2012 : Hifadhi ya Taifa ya Hell's Gate
- 01 Septemba 2012 : Ziwa Nakuru
- 01 Oktoba 2012 : Hifadhi ya Taifa ya Tsavo Mashariki
- 01 Novemba 2012 : Hifadhi ya Serengeti
- 01 Desemba 2012 : Chuo Kikuu cha Addis Ababa
Makala iliyochaguliwa kwa Aprili 2012[hariri chanzo]
Kampeni za Afrika ya Mashariki ulikuwa mfululizo wa mapigano ya kivita yaliyotokea Afrika ya Mashariki ya Kijerumani (Tanganyika, Rwanda na Burundi ya leo) na koloni jirani za Msumbiji, Rhodesia ya Kaskazini (Zambia), Afrika ya Mashariki ya Kiingereza (Kenya), Uganda, na Kongo ya Kibelgiji. Kampeni hizi zilianza mwezi wa Agosti 1914 zikaisha rasmi mnamo mwezi wa Novemba katika mwaka wa 1918. Wapiganaji katika vita hii walikuwa jeshi la kikoloni cha Kijerumani lililofanywa hasa na askari Waafrika waliosimamiwa na maafisa Wajerumani pamoja na walowezi Wajerumani na wanamaji wa manowari waliokaa Afrika ya Mashariki wakati wa mwanzo wa vita 1914. Dhidi yao walisimama jeshi dogo la kikoloni la Kiingereza katika Kenya na Rhodesia, halafu vikosi vya jeshi la kikoloni la Uhindi ya Kiingereza na vikosi kutoka Afrika Kusini.