Jamhuri ya Kongo
Jamhuri ya Kongo | |
---|---|
République du Congo (Kifaransa) Republíki ya Kongó (Kilingala) Repubilika ya Kôngo (Kituba) | |
Kaulimbiu ya taifa: Unité - Travail - Progrès (Kifaransa) "Umoja - Kazi - Maendeleo" | |
Wimbo wa taifa: La Congolaise (Kifaransa) "Wakongo" | |
Mahali pa Jamhuri ya Kongo | |
Ramani ya Mikoa ya Jamhuri ya Kongo | |
Mji mkuu na mkubwa nchini | Brazzaville 4°16′S 15°17′E / 4.267°S 15.283°E |
Lugha rasmi | Kifaransa |
Lugha za taifa | |
Serikali | Jamhuri |
Rais | Denis Sassou-Nguesso |
Uhuru kutoka Ufaransa | 15 Agosti 1960 |
Eneo | |
• Eneo la jumla | km2 342,000 |
• Maji (asilimia) | 1.5 |
Idadi ya watu | |
• Kadirio la 2023 | 6,355,235 [1] |
• Sensa ya 2023 | 6,142,180[2] |
Sarafu | Faranga ya CFA (XAF) |
Majira ya saa | UTC+1 (Afrika Magharibi) |
Msimbo wa simu | +242 |
Msimbo wa ISO 3166 | CG |
Jina la kikoa | .cg |
Jamhuri ya Kongo ni nchi ya Afrika ya Kati. Imejulikana pia kama Kongo-Brazzaville (kutokana na mji mkuu) kwa kusudi la kutoichanganywa na nchi jirani ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
Jamhuri ya Kongo imepakana na Gabon, Kamerun, Jamhuri ya Afrika ya Kati, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Angola na Bahari ya Atlantiki.
Nchi ilikuwa koloni la Ufaransa hadi tarehe 15 Agosti 1960.
Historia
[hariri | hariri chanzo]Wakazi wa kwanza huaminiwa kuwa wawindaji wa jamii ya Wasani na ya Wabilikimo.
Katika karne za BK walifika wahamiaji Wabantu wenye ujuzi wa kilimo na uhunzi waliotawala eneo lote na kuendesha biashara katika beseni ya mto Kongo.
Baadaye eneo hilo lilikuwa sehemu ya koloni la Afrika ya Kiikweta ya Kifaransa
Baada ya uhuru tarehe 15 Agosti 1960 nchi ilitawaliwa na Wakomunisti tangu mwaka 1970 hadi 1991.
Kuanzia mwaka 1992 zilifanyika chaguzi kwa mfumo wa vyama vingi, lakini mwaka 1997 vilitokea vita vya wenyewe kwa wenyewe.
Rais Denis Sassou Nguesso ametawala miaka 36 kati ya 41 ya mwisho.
Watu
[hariri | hariri chanzo]Sehemu kubwa ya nchi ni misitu, hivyo wakazi wengi (70%) wanaishi mijini upande wa kusini-magharibi wa nchi. Kati yao, 48% ni wa kabila la Wakongo, 20% Wasangha, 17% Wateke, 12% Wam'Bochi. 2% ni Wabilikimo.
Nchi ina lugha 62 tofauti, zikiwemo lugha 2 za taifa: Kingala na Kikongo (Kituba). Hata hivyo lugha rasmi ni Kifaransa.
Wakazi wengi ni Wakristo (87.1%), wakiwemo Waprotestanti (51.4%) na Wakatoliki (33.1%), ingawa asilimia zinazotajwa hazilingani. Waislamu ni 1.2%, wafuasi wa dini asilia za Kiafrika ni 2.7% na wa Baha'i 0.4%.
Tazama pia
[hariri | hariri chanzo]- Orodha ya nchi kufuatana na wakazi
- Orodha ya nchi za Afrika kulingana na idadi ya watu
- Orodha ya nchi za Afrika kulingana na msongamano wa watu
- Orodha ya nchi za Afrika kulingana na pato la taifa
- Demografia ya Afrika
- Orodha ya lugha za Jamhuri ya Kongo
- Mto Niger
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ "Republic of the Congo Population 2024 (Live)". worldpopulationreview.com. Iliwekwa mnamo 2024-08-24.
- ↑ BOKOLO, Guilesse (2024-01-08). "RESULTATS PRELIMINAIRES". INS-CONGO BRAZZAVILLE (kwa Kifaransa). Iliwekwa mnamo 2024-08-24.
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- Serikali
- Congolese Government Portal (Kifaransa)
- Presidency of the Republic Ilihifadhiwa 22 Desemba 2010 kwenye Wayback Machine. (Kifaransa)
- Chief of State and Cabinet Members
- Taarifa za jumla
- Country Profile from BBC News
- Republic of the Congo entry at The World Factbook
- Republic of the Congo Ilihifadhiwa 7 Desemba 2008 kwenye Wayback Machine. from UCB Libraries GovPubs
- Jamhuri ya Kongo katika Open Directory Project
- Wikimedia Atlas of the Republic of the Congo
- Review of Congo by the United Nations Human Rights Council's Universal Periodic Review, May 6, 2009.
- Humanitarian news and analysis from IRIN – Congo
- Utalii
Nchi za Afrika | |
---|---|
Afrika ya Kati (Jamhuri ya) | Afrika Kusini | Algeria | Angola | Benin | Botswana | Burkina Faso | Burundi | Cabo Verde | Chad | Cote d'Ivoire | Eritrea | Eswatini | Ethiopia | Gabon | Gambia | Ghana | Guinea | Guinea Bisau | Guinea ya Ikweta | Jibuti | Kamerun | Kenya | Komori | Kongo (Jamhuri ya) | Kongo (Jamhuri ya Kidemokrasia ya) | Lesotho | Liberia | Libya | Madagaska | Malawi | Mali | Misri | Morisi (Visiwa vya) | Mauritania | Moroko | Msumbiji | Namibia | Niger | Nigeria | Rwanda | Sahara ya Magharibi | Sao Tome na Principe | Senegal | Shelisheli | Sierra Leone | Somalia | Sudan | Sudan Kusini | Tanzania | Togo | Tunisia | Uganda | Zambia | Zimbabwe | |
Maeneo ya Afrika ambayo ni sehemu za nchi nje ya Afrika | |
Hispania: Kanari · Ceuta · Melilla | Italia: Pantelleria · Pelagie | Ufaransa: Mayotte · Réunion | Uingereza: · St. Helena · Diego Garcia | Ureno: Madeira |
Makala hii kuhusu maeneo ya Afrika bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Jamhuri ya Kongo kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |