Nenda kwa yaliyomo

Wikipedia:Kona ya majadiliano/Jalada 1

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Ujumbe za Category na namna zililivyo kwa Kiing.

Nikiwa bado najaribu kutafsiri baadhi ya maneno kutoka Kiingereza kuja Kiswahili huko katika BetaWiki, kuna orodha hii ya Category ambazo sijazielewa namna zilivyo. Hivyo naomba mutoe mchango wenu katika kuziita jamii hizi:

  1. Category tree
  2. Dynamically navigate the [[Special:CategoryTree|category structure]]

Bado sijaelewa kwanini wanaziita Category tree?--Mwanaharakati (Longa) 13:56, 15 Desemba 2008 (UTC)[jibu]

Category tree ni "mfumo wa jamii". Wanaiita "mti" kwa sababu mfumo hufanana mti: Jamii:Jamii Kuu ni kama mzizi au shina, halafu kuna matawi makuu (jamii 15 ambayo yanaanza moja kwa moja kwenye "Jamii Kuu"). Matawi makuu haya kuna tena matawi madogo zaidi yanayotoka; mfano: Tawi kuu Jamii:Sayansi lina tena matawi 15 madogo zaidi. Moja kati ya haya ni "Jamii:Kemia" ina tena jamii 5 zinazotoka hapa; moja ni "jamii:metali" na hii tena ina matawi 3 ambayo ni jamii:Metali adimu, jamii:metali alikali na Jamii:Metali za udongo alikalini. Nikihesabu hadi hapa kuna ngazi 5. Zinaweza kuwa zaidi. --Kipala (majadiliano) 15:56, 15 Desemba 2008 (UTC)[jibu]
Sawa. Nimekuelewa, lakini bado ninakitendawili komajo: CATEGORY TREE isimame kama "mfumo wa jamii" au "jamii kuu"?--Mwanaharakati (Longa) 16:27, 15 Desemba 2008 (UTC)[jibu]
Naona iwe "Mfumo wa jamii" pekee. Maana ukiingiza jamii yoyote dirishani unaona jamii ndogo zake na jamii ya/za juu. Jamii kuu unaona tu ukiiandika mle au jamii za ngazi ya kwanza. --Kipala (majadiliano) 17:46, 15 Desemba 2008 (UTC)[jibu]
Basi nitaweka hiyo kule BetaWiki.--Mwanaharakati (Longa) 05:50, 16 Desemba 2008 (UTC)[jibu]

Nimetafsiri, lakini kufika hapa nimekwama!

  • Dynamically navigate the [[Special:CategoryTree|category structure]]

Msaada, tafadhalini wakubwa zangu--Mwanaharakati (Longa) 06:39, 16 Desemba 2008 (UTC)[jibu]

Ukurasa gani? Anwani? --Kipala (majadiliano) 08:22, 16 Desemba 2008 (UTC)[jibu]
Yaani hivi, kule katika BetaWiki ukiwa unatafsiri jumbe za mediawiki huwa zinajiweka kwa mfululizo. Yaani ukitoka huu, unakuja huu! Angalia hapa utaona hayo maandishi ya Dynamically navigate the [[Special:CategoryTree|category structure]] yapo sehemu ya kwanza. Ninachotaka kujua ni hayo maelezo, yaani Dynamically navigate the category structure kwa tafsiri iliyoshiba! Nimeeleweka?--Mwanaharakati (Longa) 12:07, 16 Desemba 2008 (UTC)[jibu]
Nisipokosei ni "Pitilia" tu, au "Chungulia kwenye mfumo wa jamii" --Kipala (majadiliano) 17:10, 16 Desemba 2008 (UTC)[jibu]

Kutafsiri jumbe

Natafuta istilahi sahihi na zinazoeleweka kwa ajili ya jumbe. Nitashukuru kupata mawazo yenu kuhusu makendekezo yafuatavyo:

Tukikubaliana tafsiri nitayaweka kule translatewiki.net. Jumbe mpya zitafika hapa wikipedia ya kiswahili baada ya siku au wiki chache. Ikihitajika maelezo mengine kuhusu utumiaji wa jumbe hizi na maana ya Kiingereza nitaeleza zaidi. Lloffiwr (majadiliano) 22:23, 22 Februari 2009 (UTC)[jibu]

Tayari:

  • Search results - matokeo ya utafutaji
  • Search the pages for this text - 'tafuta kurasa kwa maandishi haya'.
  • newer - ya karibu zaidi
  • older - ya zamani zaidi
  • view source - sasa hivi ni 'tazama chanzo' - tazama mfano wa [1] (kwenye 'tab' juu ya ukurasa). Je, inaridhisha?
    • Mwanaharakati amependekeza 'Onyesha kodi za ukurasa'. Mnaonaje? Lloffiwr (majadiliano). 'Onyesha kodi za ukurasa. imewekwa.
  • Namespace - sasa hivi ni 'eneo la majina' - tazama Special:AllPages. Nina wasiwasi na hilo 'eneo la majina'. Mifano ya 'namespace' ni - 'kuu', 'mtumiaji', 'majadiliano ya mtumiaji', 'jamii'. Yaani, kuna eneo kuu, eneo la watumiaji, eneo la majadiliano ya watumiaji, eneo la jamii, na kadhalika. Sasa, nikisoma 'eneo la majina' najiuliza - huu ni eneo gani? Sasa ni eneo la wiki.
  • MediaWiki:Lastmodifiedat ukurasa huu umebadilishwa kwa mara ya mwisho tarehe $1, saa $2.
    • [2] Ukurasa huu ulibadilishwa mwishoni saa $2, tarehe $1 na $3.

Bado:

  • redirect - sasa hivi ni 'elekeza'. Je, 'chepuza' ni bora?
  • Content pages - hapa Wikipedia hizi ni makala na picha zinazoonekana kwenye makala; yaani, ni kurasa zile za nia ya wiki. Hata kwenye Kiingereza jina hili la 'Content pages' halieleweki kirahisi. Wanatumia jina hili kule Wikimedia wakati wanataka kutofautishana kati ya kurasa ambazo ni sehemu ya nia ya wiki (content pages), na kurasa nyingine kama kurasa ya majadiliano, kurasa ya jamii, na kurasa nyingine ambazo ni za kusaidia katika kujenga kurasa za 'content pages'. 'Content pages' huwa zipo ndani ya 'namespace' 'kuu' au 'namespace' mafaili.
  • Lloffiwr (majadiliano) 19:09, 7 Machi 2009 (UTC)[jibu]

Jumbe ya matangazo

Kuna jumbe ya 'site notice' (tangazo pembeni mwa ukurasa) ambayo ninapendekeza kuyatafsiri hivyo.

  • Hide
    • Ficha = ndiyo
  • Show
    • Onyesha = ndiyo
  • Help us with translations!
    • Tusaidie kutafsiri! = ndiyo

Je, mapendekezo haya yanaridhisha? Lloffiwr (majadiliano) 11:18, 14 Machi 2009 (UTC)[jibu]

Maelezo yote yako sahihi. Chukua hatua tu!--Mwanaharakati (Longa) 11:38, 14 Machi 2009 (UTC)[jibu]
Kumbe. Help us with translations imeshatafsiriwa kule Meta na Baba Tabita. Ametafsiri 'Utusaidie kutafsiri!' Ujumbe utabadilishwa kule Meta hivi karibuni nadhani. Lloffiwr (majadiliano) 12:17, 14 Machi 2009 (UTC)[jibu]
Tayari. Lloffiwr (majadiliano) 19:47, 14 Machi 2009 (UTC)[jibu]

Mapinduzi ya ukurasa wa mwanzo

Salama Wanawikipedia wote. Hizi ni taarifa kuhusu kuumba upya ukurasa wa mwanzo wa Wikipedia yetu! Ingawa kazi hii inaonekana kutokuwa rahisi, lakini bado tunatakiwa tukabiliane na hili. Kwa mtazamo wangu binafsi (pia nikipata mawazo kutoka kwa Wanawikimedia wengine) juu ya mawazo ya kubadilisha au kuumba upya ukurasa wa mwanzo wa Wikipedia yetu - wanadai kwamba ipo kizamani sana. Jambo ambalo si la kawaidai kwa Wikipedia zilizonyingi. Tangu tuanze kuutumia ukurasa huu, sasa yapita takriban miaka minne au mitano! Ninaomba Wanawikiedia wote wanaoshirki hapa tuungane kuubadilisha ukurasa wa mwanzo wa Wikipedia yetu.


UKURASA MPYA KUTOKA EN:WIKI NA KUULETA KWENYE MAZINGIRA YA KISWAHILI

Karibu kwenye Wikipedia,
kamusi elezo huru, kila mtu anaweza kuihariri!
Hadi leo tuna makala takriban 90,685 kwa Kiswahili
     

     

Kamusi Elezo ya Kiswahili

Karibu kwenye Wikipedia ya Kiswahili!

Wikipedia ni mradi wa kuandika kamusi elezo kamili na sahihi ya maandishi huru.

Kila mtu anaweza kuhariri makala yoyote, kutoa makosa ya lugha, kutohoa maneno na kuendeleza na kukuza makala, kwa kuandika kwa ufupi au kwa urefu. Tunakushauri ujiandikishe na kufungua akaunti. Angalia Wikipedia:Mwongozo ili ujifunze unavyoweza kuhariri au kusanifisha ukurasa. Usisite kushiriki; kwa sababu huu ni mradi wa ushirikiano, na hautaisha kamwe. Kamusi elezo itaimarika vizuri zaidi kila wakati. Angalia ukurasa wa jumuia, ukurasa wa jamii, na ule wa makala za msingi za kamusi elezo ili kung'amua unaweza kufanya kazi zipi ili kuboresha Wikipedia.


Je, wajua...

Kutoka kwenye mkusanyiko wa makala za Wikipedia:

Ngorongoro

  • ... kwamba Hifadhi ya Ngorongoro imepokewa katika orodha ya urithi wa dunia ya UNESCO?
  • ... kwamba Asha-Rose Mtengeti Migiro ni mwanasiasa wa kwanza kutoka nchini Tanzania aliyepata kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa?
  • ... kwamba Septemba 1752 ilikosa siku kumi na moja? Katika Dola la Uingereza, ulikuwa mwaka pekee wenye siku 355, kwani Septemba 3-13 zilirukwa wakati Dola lilipopitisha kalenda ya Gregori.
  • ... kwamba Samia Hassan Suluhu ni rais wa kwanza mwanamke Afrika ya Mashariki? Aliapishwa kuwa rais mara baada ya kifo cha mtangulizi wake, John Pombe Magufuli.


  • Makala ya wiki

    Kassim Mapili

    Kassim Said Mapili (1937 - 2016) alikuwa mwanamuziki maarufu wa muziki wa dansi kutoka nchini Tanzania. Mzee Mapili alizaliwa katika kijiji cha Lipuyu, Tarafa ya Lionya, Wilaya ya Nachingwea mkoani Lindi mwaka 1937. Hivyo umauti umekuta Mzee Mapili akiwa na umri wa miaka 79. Alipata elimu ya msingi huko kwao Lipuyu, sambamba na kupata elimu ya dini na mwenyewe aliwahi kusema alianza kupata mapenzi ya kuimba wakati alipokuwa Madrasa akighani Kaswida. Mwaka 1958 alijiunga na White Jazz Band iliyokuwa na masikani yake huko Lindi.

    Mwaka mmoja baadaye akahamia Mtwara na kujiunga na Mtwara Jazz Band, lakini mwaka 1962 akajiunga na Honolulu Jazz Band ambayo nayo ilikuwa hapo hapo Mtwara. Mwaka 1963, Mzee Mapili akachukuliwa na TANU Youth League ya mjini Lindi, na kujiunga na bendi ya Jamhuri Jazz Band ya hapo Lindi. Mwaka 1964 Mzee Mapili akachaguliwa kuanzisha bendi ya TANU Youth League ya Tunduru. Mwaka mmoja baadaye alihamia Kilwa Masoko na kujiunga na Lucky Star Jazz Band ya mji huo. ►Soma zaidi


    Picha nzuri ya wiki

    Samia Sulu Hassan

    Samia Suluhu Hassan ni rais wa sita wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Picha hii ni 2011 akiwa Ubalozi wa Marekani, Dar es Salaam.

    Jumuia za Wikimedia

    Commons
    Ghala ya Nyaraka za Picha na Sauti
    Meta-Wiki
    Uratibu wa Miradi yote ya Wikimedia
    Wikamusi
    Kamusi na Tesauri
    Wikitabu
    Vitabu vya bure na Miongozo ya Kufundishia
    Wikidondoo
    Mkusanyiko wa Nukuu Huria
    Wikichanzo (Wikisource)
    Matini za vyanzo asilia kwa Kiswahili
    Wikispishi
    Kamusi ya Spishi
    Wikichuo
    Jumuia ya elimu
    Wikihabari
    Habari Huru na Bure


    Maelezo

    Haya, tuachague maelezo ya kutoa katika orodha ya vichwa vya habari husika na maelezo tajwa hapo juu. Binafsi naonelea kuondoa maelezo yalipo chini ya mstari ulioandikwa:

    Overview · Editing · Questions · Help Contents · Categories · Featured content · A–Z index

    Sizani kwamba mstari huu hapa kwetu kama una muhimu kabisaa. Kwa sasa bado ninaendelea kuumba baadhi ya vigezo vilivyoonekana mule katika VICHWA VYA HABARI.--Mwanaharakati (Longa) 08:46, 15 Mei 2009 (UTC)[jibu]

    Ningependa kwamba viungo vya Jamii na Kurasa zote vibaki. Lloffiwr (majadiliano) 12:50, 25 Mei 2009 (UTC)[jibu]
    Kwenye sehemu ya 'miradi ya wikipedia sister' viungo vyote ni kwenye miradi ya kiingereza. Lakini mradi wa wiktionary upo ila bado ndogo. Kwa hiyo labda tubadilishe kiungo iende kwenye Wikamusi ya kiswahili? 91.125.92.78 14:58, 16 Mei 2009 (UTC)[jibu]
    Nimeona. Kumbe inaenda kweli Kiingereza. Lakini si ndogo sana - maana ni ya 46 kwa ukubwa! Nitabadilisha..--Mwanaharakati (Longa) 15:18, 16 Mei 2009 (UTC)[jibu]
    Je, nadhani kwamba sehemu za 'katika siku hizi', 'je, wajua', na 'picha nzuri ya wiki' zitakuwa vigumu kutengeneza pamoja na kurekebisha kila wakati. Je, tuondoe sehemu hizi hadi tutakapopata picha, makala na watu wa kutosha kuyatengeneza? Au labda sehemu ya 'je, wajua', ingeweza kuwekwa, ambaye itabaki ilivyo kwa muda mrefu. Lloffiwr (majadiliano) 12:50, 25 Mei 2009 (UTC)[jibu]
    Enhee! Je, wajua, ni bora tuiache bimaana kwamba tutaiweka labda mara moja kwa mwezi. Kuhusu picha, sio lazima zitoke hapa kwani hata tukichukua kutoka commons, sawa.. Je, kuhusu hizo sehemu tutakazozitoa tutazijaza vipi?--Mwanaharakati (Longa) 13:59, 25 Mei 2009 (UTC)[jibu]
    Sehemu tutakazozitoa zinaweza kubaki wazi, je? Kuhusu picha, ni kweli kwamba picha zinaweza kutoka Commons. Huwa, kwenye Wikipedia ya Kiingereza, picha zinatoka Commons lakini wanachagua picha inayotumika kwenye Wikipedia, na kuweka muhtasari wa makala moja inayotumia picha kando ya picha yenyewe. Tunaweza kufanya vilivile hapa - wasiwasi wangu ni kuhusu ukubwa wa kazi ya kubadilisha badilisha picha. Kubadilisha kila mwezi si mbaya. Hata hivyo, ni kweli kwamba kwenye wiki zingine wanaonyesha picha toka Commons kwenye ukurasa wa mwanzo, bila kuweka muhtasari ya makala inayotumia ile picha.
    Kwenye wikipedia zingine, wanaorodhesha makala yalioonyeshwa kwenye ukurasa wa mwanzo kwenye ukurasa wa pekee, na kiungo kutoka ukurasa wa kwanza, ili watu waweze kuona makala mengine yaliyochaguliwa awali yaonyeshwe kwenye ukurasa wa kwanza - tazama wikipedia ya occitan. Na vilevile kwa ajili ya picha - tazama wikipedia ya esperanto. Lloffiwr (majadiliano) 16:29, 25 Mei 2009 (UTC)[jibu]
    Hongera Bwana Mwanaharakati! Nakushukuru tele kwa kazi hizo ambazo nisingekuwa na nafasi kuzifanya. Endelea tu. Nakuunga mkono moja kwa moja! Wasalaam, --Baba Tabita (majadiliano) 06:48, 27 Mei 2009 (UTC)[jibu]
    Kumbe kazi kubwa! Naona sawa tu ukiendelea kubadilisha asante kwa kutuonyesha kwanza! Mawazo machache: Sehemu ya "Karibu kwenye Wikipedia ya Kiswahili!" afadhali upande wa kushoto kwa sababu hapo tunaanza kusoma. Sehemu ya "Jumuiya ya wikipedia" inachukua nafasi kubwa hapa nina wasiwasi kwa sababu hatutakuwa na miradi hii mingine karibuni. Kwa hiyo kama inasaidia kupunguza maandishi labda kutafuta njia ya kupunguza nafasi kubwa ya sehemu hii. Commons na Meta zikae mwanzoni kwa sababu ni hizi zenya maana zaidi lakini mengine hazituhusu sana. ----Kipala (majadiliano) 20:26, 27 Mei 2009 (UTC)[jibu]
    Haya, nimebadilisha ule utangulizi wa Kamusi Elezo kuwa upande wa kushoto kama jinsi alivyoshauri Mzee Kipala. Kuhusu kupunguza ukubwa sehemu ya kuorodheshea miradi ya Wikimedia, naonelea yule Mwelisi (Lloffiwr) yeye atafikiria namna ya kupunguza ili isichukue nafasi kubwa kama ile. Pia, ninaona ulazima kutoandika kipengele kikubwa cha makala ya wiki - kwani ile ndiyo inayosababisha urefu wote wa ukurasa huu. Sivyo?--Mwanaharakati (Longa) 14:51, 29 Mei 2009 (UTC)[jibu]
    Nimepunguza ukubwa wa maandishi kwenye sehemu ya 'Jumuia ya Wikimedia' pamoja na kusogeza Commons na Meta. Nimepunguza ukubwa wa maandishi kwenye sehemu ya 'Wikipedia kwa lugha nyingine' pia. Naweza kuzibadilisha tena zisipopendeza (sasa hivi ni 80%). Mnaonaje?
    Nakubali makala ya wiki iwe ndogo zaidi - ukurasa ni mrefu na bado kuna sehemu zingine hazijatengenezwa. Ninapolinganisha sura ya Wikipedia ya Kiswahili na za lugha zingine naona kwamba maandishi ya Kiswahili ni kubwa. Ninafikiri kwamba ni lazima kubadilisha faili kuu ya lugha, faili ya .php ili kubadilisha ukubwa wa maandishi wa wikipedia ya Kiswahili kwa ujumla, lakini sina ujuzi wa kufanya hivyo. Lloffiwr (majadiliano) 19:27, 30 Mei 2009 (UTC)[jibu]
    Haya, nami nimeona badiliko lako. Limeleta maana kwa kiasi kikubwa kabisa. Nami nimejaribu kuanzisha baadhi ya MILANGO, yaani, PORTAL, lakini nilivyofika kwenye Mlango wa Historia, Sayansi, na... Nimeshindwa kuanzisha milango yake. Badala yake nikaelekeza kila Mlango katika makala husika na Mlango huo. Picha ya wiki? Si tatizo. Tatizo ni katika kuumba JE WAJUA? Hii inataka ushirikiano wa Wanawikipedia tuliopo humu kwetu! Itakuwa vyema tukiwa tunatumia ukurasa wa majadiliano wa kipengele husika (Majadiliano:Je Wajua). Tunaandaa mapendekezo kisha tunayaweka kwenye mahala pake. Haya jamani tujitahidi angalau kwenye mwezi wa Julai ukurasa wetu mkuu uwe ushabadilishwa. Kila la kheri.--Mwanaharakati (Longa) 16:00, 15 Juni 2009 (UTC)[jibu]