Vwawa

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru


Jimbo la Vwawa
Nchi Tanzania
Mkoa Songwe
Wilaya Mbozi
Idadi ya wakazi
 - Wakazi kwa ujumla 56,256

Vwawa ni jina la mji na makao makuu ya Wilaya ya Mbozi katika Mkoa wa Songwe, pia ni jimbo la uchaguzi nchini Tanzania.

Mji huo unapatikana Nyanda za Juu za Kusini mkoa mpya wa Songwe (zamani sehemu ya mkoa wa Mbeya) tena na ni makao makuu ya mkoa huo.

Wakati wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ya Vwawa ilikuwa na wakazi wapatao 56,256 [1] walioishi humo. Msimbo wa posta ni 53301.

Asili ya jina la Vwawa ni mtemi au mlima.

Mji huu uko kando ya barabara kuu kupitia mikoa ya Mbeya, Njombe, Iringa, Morogoro, Pwani kutokea jijini Dar es Salaam. Barabara hiyo inakwenda Zambia na Malawi kupitia wilaya ya Ileje na mkoa wa Rukwa.

Mji huu umepitiwa pia na reli ya TAZARA kutokea jijini Dar es Salaam hadi Kapiri Mposhi nchini Zambia.

Mji huu una wenyeji ambao ni Wanyiha, Wandali na Wanyamwanga na baadhi ya Wanyakyusa wapatikanao katika maeneo ya masoko na Ndolezi wilayani Mbozi, lakini pia makabila mengine ambayo si asili katika wilaya ya Mbozi.

Mji huu una mitaa yake ambayo ni: Old Vwawa, Ilolo, Mwenge, Ichenjezya, Ilembo, Frolida, Mbimba Itemba, Mtambwe, Jim road, Isangu, Ichenjezya, Mbugani, Vwawa day na Masaki.

Mji huu umetoa wasomi wengi sana ambao ni chachu ya maendeleo kwa nchi ya Tanzania.

Mji huu umezungukwa na huduma mbalimbali za kijamii ikiwemo za serikali na watu binafsi kama vile shule, hospitali, nyumba za serikali, benki na huduma nyingine kama vile vituo vya mafuta, masoko, maji ya kutosha na umeme.

Mji huu una ardhi nzuri ambayo si ya hali ya ukame na ambayo inaruhusu uwepo wa vyakula vya aina nyingi kwa vipindi vyote, yaani kiangazi na masika.

Mlima Ng'amba na milima mingine ionekanayo kwa umbali ni kati ya vitu vioneshayo Vwawa kwa uzuri wa kipekee.

Kazi nzuri ifanywayo na jeshi la polisi pamoja na ukarimu pia ushirikiano wa watu wa Vwawa vimefanya Vwawa kuwa mji wenye utulivu muda wote.

Hata hivyo, mnamo mwaka 2015 jina la Vwawa liliingia katika vichwa vikuu vya habari nchini Tanzania baada ya kuhusishwa na harakati za kuufanya kuwa makao makuu ya mkoa mpya wa Songwe kabla ya kupitishwa kwake rasmi mnamo mwaka 2016.

Uwepo wa kampuni binafsi kama vile Ilasi, Unyiha, ADP na nyingine nyingi umesaidia sana sekta za elimu, uchumi, habari na masuala ya kilimo.

Pia Vwawa inatoa fursa ya uwekezaji kwa wageni na wenyeji katika masuala mbalimbali. Wenyeji wa mji huu wa Vwawa wanawakaribisha sana wageni wa mikoa na wilaya nyingine ili kuwezesha mzunguko wa kibiashara na wa kijamii.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. Sensa ya 2012, Mbeya - Mbozi DC. Jalada kutoka ya awali juu ya 2016-03-03. Iliwekwa mnamo 2017-03-13.
Kata za Wilaya ya Mbozi - Mkoa wa Songwe - Tanzania

Bara | Halungu | Hasamba | Hasanga | Hezya | Ichenjezya | Idiwili | Igamba | Ihanda | Ilolo | Ipunga | Isalalo | Isansa | Itaka | Itumpi | Iyula | Kilimampimbi | Magamba | Mahenje | Mlangali | Mlowo | Msia | Nambinzo | Nanyala | Nyimbili | Ruanda | Shiwinga | Ukwile | Vwawa


Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Songwe bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Vwawa kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari .
Usiingize majina ya viongozi au maafisa wa sasa maana wanabadilika haraka mno