Vita ya miaka 30

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Jeshi la Kaisari mbele ya Stralsund
Mapigano kwenye daraja la Prague 1648
Ulaya baada ya Amani ya Westfalia

Vita ya miaka 30 ilipiganiwa kati ya 1618 hadi 1648. Ilikuwa vita ya Kiulaya lakini mapigano yake yalitokea hasa katika Ujerumani kwenye eneo la Dola Takatifu la Kiroma. Madola ya Ujerumani yalipigana kati yao na nchi za nje zilishiriki pamoja na Hispania, Ufaransa, Uswidi, Uholanzi na Denmark.

Vita ilileta uharibifu kupita kiasi kwa ajili ya Ujerumani kushinda vita zote zilizofuata katika historia. Hukumbukwa hadi leo.

Hali ya kisiasa kabla ya vita[hariri | hariri chanzo]

Ujerumani ilikuwa sehemu kubwa ya Dola Takatifu la Kiroma pamoja na majimbo ambayo leo ni Ucheki, Uholanzi, Uswisi, Ufaransa ya magharibi, Italia ya kaskazini na Austria. Dola Takatifu ilikuwa kama maungano ya madola madogo zaidi chini ya Kaisari.

Mkuu alikuwa Kaisari aliyetoka katika nasaba ya Habsburg akiwa mtawala wa Austria hasa na madaraka yake juu ya Dola Takatifu kwa jumla yalikuwa madogo. Maneeo mengine yalijitegemea kwa kiasi kikubwa chini ya watawala wao wa kikabaila. Miaka 100 kabla ya vita mategenezo ya Kiprotestant yalienea katika Ujerumani na sehemu ya madola ilipokea dhehebu jipya lakini wengine walikuwa Wakatoliki. Madola mengi yalisisitiza ya kwamba wanachi wote wafuate dhehebu moja tu hapakuwa na uhuru wa kidini kwa kila raia.

Fitina ya kidini katika Bohemia[hariri | hariri chanzo]

Vita ilianza kama fitina kati ya Kaisari aliyekuwa Mkatoliki Mwaustria na maungano ya madola ya Kiprotestanti ndani ya Dola Takatifu. Chanzo kilikuwa uasi wa makabaila wa Kiprotestanti katika jimbo la Bohemia dhidi ya siasa ya Kaisari Ferdinand II aliyechaguliwa pia kuwa mfalme wa Bohemia.

Ferdinand alikataa kukubali uhuru wa kidini ulioahidiwa na mtangulizi wake kwa ajili ya Bohemia. Fitina hii ilikuwa vita baada ya gavana wa Kaisari kutupwa nje ya dirisha la chumba cha mkutano mjini Praha tar. 23 Mei 1618. Wakubwa wa Bohemia waliendela kutamka ya kwamba Ferdinand si mfalme wao tena wakamchagua mkabaila wa Palentino kama mfalme mpya.

Kaisari alichukua silaha na kwneye mapigano ya kwanza ya vita tar. 8 Novemba 1619 karibu na mji wa Praha waasi wa Bohemia walishindwa. Makabaila wengi wa Kiprotestant kutoka madola mengine ya Ujerumani waliamua kuwasaidia wenzao wa Bohemia. Vita hii ilielekea kwisha kwa ushindi wa Kaisari mnamo 1623.

Uswidi kusaidia Waprotestanti[hariri | hariri chanzo]

Hapa nchi jirani zilijiunga na vita. Nchi za Skandinavia zilifuata Uprotestanti na watawala wao waliamua kuwasaidia wenzao Wajerumani. Wadenmark kwanza halafu Waswedi walifika kwa wanajeshi wengi. Mfalme Gustav Adolf wa Uswidi alishinda jeshi la Kaisari mara kadhaa hadi alipouawa kwenye mapigano ya Lützen tar. 16 Novemba 1632.

Kuingilia kwa Ufaransa[hariri | hariri chanzo]

Baada ya kuona ya kwamba Kaisari aliendelea kusogea mbele mfalme wa Ufaransa alijiunga na Uswidi akashiriki katika vita tangu 1635. Nia yake ilikuwa hasa kuzuia enzi ya nasaba ya Habsburg iliyotawala Hispania ikashika pia Austria pamoja na cheo cha Kaisari wa Dola Takatifu la Kiroma. Hivyo vita iliyoanza kama mapigano ya kidini katika dola moja la Ujerumani iliendelea kuwa vita ya Kiulaya ambako nchi ya Wakatoliki kama Ufaransa ilishikamana na Usidi ya Kiprotestanti dhidi ya Kaisari Mkatoliki.

Vita lilileta uharibufu mno katika Ujerumani. Kuna makadirio ya kwamba karibu theluthi moja ya wakazi wote walikufa kutokana na mauaji, njaa na magonjwa. Katika maeneo ya Ujerumani ya Kusini zaidi ya nusu ya watu walipotea. Wanajeshi walikuwa askari wa kukodiwa ambao mara nyingi hawakulipiwa wakapewa uhuru wa kutwaa chochote walichotaka kwa mabavu.

Amani ya Westfalia[hariri | hariri chanzo]

Uchofu ulileta majadiliano juu ya amani. Mwaka 1648 wawakilishi wa wafalme walipatana katika amani ya Westfalia kanuni za amani.

  • Madhehebu matatu yalikubaliwa katika Ulaya ni Wakatoliki, Waluteri na Wareformed.
  • Kila mtawala aliamua kwa dola lake ni dini lipi litafuatwa lakini raia walikuwa na haki ya kutoka katika nchi kama mtawala alikataa dini yao. Sheria ilikuwa: "Cuius regio eius religio" (mwenye nchi ni mwenye kuamua dini)
  • Uholanzi na Uswisi zilitoka katika Dola Takatifu la Kiroma kama nchi huria za pekee.
  • Mfalme wa Uswidi alitwaa maneneo makubwa katika Ujerumani ya KAskazini