Amani ya Westfalia

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Ulaya baada ya Amani ya Westfalia 1648;
mstari mwekundu: Eneo la Dola Mtakatifu

Amani ya Westfalia ilikuwa mapatano yaliyomaliza vita ya miaka 30 katika Ujerumani na nchi za jirani. Mapatano yalimalizika katika mikutano kwenye miji ya Münster na Osnabrück

Washiriki katika mapatano ya walikuwa Kaisari Ferdinand III wa Dola Takatifu la Kiroma, watawala wengine wa madola katika Ujerumani, Hispania, Ufaransa, Uswidi na Uholanzi.

Kati ya matokeo ya kudumu yalikuwa uhuru wa Uswisi na Uholanzi zilizohesabiwa awali kama sehemu za Dola Takatifu, mapatano kuhusu uvumilivu kati ya Wakatoliki, Walutheri na Wareformed kama madhehebu makubwa ya Kikristo katika Ujerumani na kupungukiwa kwa madaraka ya Kaisari lakini kuongezeka za haki za madola madogo ndani ya Ujerumani.

Mataifa ya nje kama Uswidi na Hispania yalikuwa sasa na maeneo ndani ya Dola Takatifu na Ujerumani penyewe; madola ya Ujerumani kama Habsburg-Austria na Brandenburg-Prussia yalitawala maeneo nje ya Dola Takatifu.