Bohemia

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Bohemia kwenye ramani ya Ucheki

Bohemia (Kicheki na Kislovakia: Čechy; Kijerumani: Böhmen; Kipoland: Czechy) ni mkoa wa kihistoria katika magharibi ya Ucheki. Jina limetokana na neno la Kilatini kwa ajili ya eneo la kabila la "Boio" ("Boiohaemum" = eneo la Waboio, baadaye: "Bohemia") lililowahi kukalia sehemu zile zamani za Roma ya Kale.

Pamoja na Moravia eneo la Bohemia ni sehemu muhimu ya Ucheki ambayo ni nchi iliyoanzishwa mwaka 1993 baada ya Slovakia kutoka katika Chekoslovakia. Bohemia imepakana na Poland upande wa kaskazini, Ujerumani upande wa kaskazini na magharibi, Austria upande wa Kusini na mkoa wa Moravia upande wa mashariki.

Mji mkuu wa Bohemia ni pia mji mkuu wa kitaifa ni Praha (Kiing.: Prague).