Usanifu majengo wa Waswahili
Usanifu majengo wa Waswahili ni usanifu wa mila mbalimbali za ujenzi zinazotekelezwa au zilizoanzishwa na Waswahili katika mwambao wa mashariki na kusini mashariki mwa Afrika. Badala ya viasili rahisi vya usanifu wa Kiislamu kutoka katika ulimwengu wa Kiarabu, usanifu huo wa majengo ulibadilika kutokana na mila za kijamii na kidini, mabadiliko ya kimazingira, na maendeleo ya miji ya asili ya Waswahili. [1]
Mifano ya usanifu majengo wa Waswahili bado inaonekana sana katika maeneo ya kale ya miji kama Bagamoyo, Mombasa, Lamu na Malindi, Songo Mnara, Kilwa Kisiwani, na miji mingi ndani ya Zanzibar nchini Tanzania. Usambazaji huu wa usanifu wa Waswahili na miji hutoa vidokezo muhimu kuhusu uhusiano wa kibiashara kati ya mikoa na mifumo mbalimbali katika jamii hiyo. [2]
Mapambo mengi ya kigeni na vipengele vya kubuni pia vinaunganisha usanifu wa asili ya pwani ya Uswahili na miji mingine ya bandari ya Kiislamu duniani pia vilichangia baadaye. Majumba mengi ya kifahari ya Waswahili na majumba ya pwani ya Uswahili yalikuwa ya wafanyabiashara tajiri na wamiliki wa ardhi, ambao walichukua jukumu muhimu katika uchumi. Usanifu majengo ya Waswahili unaonyesha ubunifu, athari, na aina mbalimbali. Historia hufungamana na kuingiliana, na kusababisha miundo yenye tabaka nene ambalo haliwezi kugawanywa katika sehemu tofauti za kimtindo zisizopatikana popote pengine duniani. Magofu mengi ya kuvutia ya kile kinachoitwa enzi ya dhahabu ya usanifu wa Waswahili bado yanaweza kuonekana karibu na bandari ya kusini mwa Kenya ya Malindi katika magofu ya Gedi. Pamoja na miji mbalimbali nchini Tanzania kama Kilwa, Tongoni na Pangani.
Vipengele muhimu
[hariri | hariri chanzo]Kando ya pwani ya Afrika Mashariki, kuna makaburi mengi ya mawe yaliyojengwa na Waswahili, pamoja na nyumba na misikiti. Waswahili walitumia chokaa cha matumbawe ili kuimarisha ujenzi sahihi wa usanifu wa Waswahili na uliimarisha utendaji wa mahitaji ya kibinadamu na mazingira halisi. [3] [4] Malighafi nyingine, ikiwa ni pamoja na matambara ya matumbawe na nguzo za mikoko hutumiwa sana kufafanua na kulinda majengo ya mawe. Miundo ya mapambo hayo kwenye nyuso za jengo imeathiriwa na mchanganyiko wa tamaduni za Afrika Bara pamoja na msukumo kutoka kwa wahamiaji kutoka Uarabuni na Uhindi. Miundo mbalimbali kwenye paa na madirisha hulinda majengo kutokana na misimu mikubwa ya monsuni za bahari ya Hindi.
Katika sifa zinazojulikana zaidi za usanifu majengo wa Waswahili ni Milango ya Waswahili. Miundo na motifu za milango hiyo inaweza kugawanywa katika aina mbili. Kwanza, fremu za mstatili zinawakilisha mtindo wa zamani za Waswahili zenye vizingiti vilivyonyooka. Aina ya pili ni linta zenye viunzi vya upinde vilienea zaidi katika karne ya 19 na baadaye. Katikati ya linta za milango hiyo mara nyingi hubeba maandishi ya Kiarabu yaliyochongwa, kama vile nukuu kutoka Kurani au habari kuhusu mwenye nyumba. Kwa hiyo, milango ya Waswahili kwa kawaida hutumika kama kiashirio muhimu cha kukuza na kuashiria hali ya kijamii ya mwenye nyumba.
Katika ngazi ya miji, miji ya Waswahili hupangwa kupitia sehemu zinazoitwa mitaa, zilizogawanywa na kuta za miji hiyo. Kila mtaa huzunguka msikiti, ambao upo katikati. Hali ya kijamii ya kila mtaa inaweza kuonyeshwa kupitia aina za majengo na shughuli zilizofunuliwa kupitia uchimbaji wa kiakiolojia.
Ukitazama ndani ya muundo wa ndani wa nyumba ya Waswahili ya kawaida, utakuta imeundwa kuzunguka ua wa kati ambao unajitosheleza. Faragha ya maisha ya Kiswahili ya nyumbani inathaminiwa, kwani nafasi ya kuishi ya wamiliki imetenganishwa na nafasi yao ya umma. Ukumbi wa ndani umeelekezwa ukuta mkubwa unaozuia mtazamo wa ua wa ndani. Ua pia hutuliza joto ndani ya jengo hilo. [5]
Tazama pia
[hariri | hariri chanzo]Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ Lauren, Samantha (2014). "Between Africa and Islam: An Analysis of Pre-Colonial Swahili Architecture". ProQuest Dissertations Publishing.
- ↑ "Stone Towns of the Swahili Coast – Archaeology Magazine". www.archaeology.org. Iliwekwa mnamo 2021-03-30.
- ↑ "Architecture of the Port". africa.si.edu. Iliwekwa mnamo 2021-03-30.
- ↑ author., Meier, Prita (2016). Swahili port cities the architecture of elsewhere. Indiana University Press. ISBN 978-0-253-01915-8. OCLC 949375681.
{{cite book}}
:|last=
has generic name (help)CS1 maint: multiple names: authors list (link) - ↑ Donley, Linda W. “Life in the Swahili Town House Reveals the Symbolic Meaning of Spaces and Artefact Assemblages.” The African Archaeological Review, vol. 5, Springer, 1987, pp. 181–92, http://www.jstor.org/stable/25130491.