Songo Mnara

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search

Songo Mnara ni kisiwa katika funguvisiwa ya Kilwa, upande wa kusini mwa Kilwa Kisiwani. Kiutawala ni sehemu ya kata ya Songosongo kwenye Wilaya ya Kilwa, Tanzania.

Upande wa mashariki wa kisiwa kuna maghofu ya mji wa kale wa Songo Mnara. Maghofu haya yamepokelewa pamoja na yale ya Kilwa Kisiwani katika orodha ya urithi wa dunia wa UNESCO.

Katika karne za 13 - 16 ilikuwa mji muhimu wa biashara ya Bahari Hindi kutokana na mabaki ya bidhaa yaliyopatikana hapa[1]. Mabaki ya dhahabu, fedha, lulu, marashi, vyombo vya Uajemi na kauri za China yalipatikana na kuonyesha upana wa biashara ya wenyeji[2].

Wataalamu wa akiolojia walitambua misikiti 6, makaburi 4, uwanja 3 na nyumba zaidi ya 20. Ujenzi ulikuwa wa matumbawe na simiti.[3]

Haijulikana ni nini iliyosababisha kuanguka wa mji huu lakini mwisho wa mabaki unalingana takriban an kufika kwa Wareno katila Afrika ya Mashariki hivyo kuna watalaamu wanaohisi mvurugo uliosababishwa na kufika kwa Wareno ulileta pia anguko la Songo Mnara.


Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. Stoetzel, Jack (2011). "Field Report: Archaeological Survey of Songo Mnara Island". Nyame Akuma 76: 9–14.
  2. Zhao, Bing (March 2012). "Global Trade and Swahili Cosmopolitan Material Culture: Chinese-Style Ceramic Shards from Sane ya Kati and Songo Mnara (Kilwa, ,Tanzania)". Journal of World History 23: 41–85. doi:10.1353/jwh.2012.0018 .
  3. Fleisher, Jeffrey; Wynne-Jones, Stephanie (2012). "Finding Meaning in Ancient Swahili Spatial Practices". African Archaeological Review 29: 171–207. doi:10.1007/s10437-012-9121-0 .


Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]

Flag of Tanzania.svg Kata za Wilaya ya Kilwa - Mkoa wa Lindi - Tanzania Flag of Tanzania.svg

ChumoKandawaleKibataKikoleKijumbiKilwa MasokoKipatimuKivinje SinginoKiranjeranjeLihimalyaoLikawageMandawaMitejaMingumbiMitoleNamayuniMiguruweNanjirinjiNjinjoPandeSomangaSongosongoTingi (Kilwa)