Mtumiaji:Zenman/Mradi wa Afrika

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search

Makala iliyochaguliwa[hariri | hariri chanzo]

Makala iliyochaguliwa kwa Julai 2012[hariri | hariri chanzo]

Assia Djebar.jpg

Assia Djebar (Kiarabu: آسيا جبار‎) ni jina la kuandika la Fatima-Zohra Imalayen (amezaliwa tar. 30 Juni, 1936), yeye ni mwandishi wa riwaya, mtafsirishaji na mtengenezeji wa filamu. Kazi zake nyingine uhusu vikwazo vinavyowakumba wanawake, na anafahamika kwa mtazamo wake wa kuunga mkono wanawake. Djebar hutazamwa kama mmoja wa waandishi maarufu zaidi na wenye ushawishi mkubwa katika eneo la Afrika Kaskazini. Aluchaguliwa kwa Académie française mnamo tarehe 16 Juni, mwaka wa 2005, mwanamke wa kwanza kutoka eneo la Maghreb kutambuliwa kwa njia hiyo. Djebar alizaliwa katika eneo la Cherchell, mji mdogo wa pwani karibu na Algiers. Familia yake iliishi katika kijiji kidogo cha karibu kilichoitwa Mouzaïaville. Pale, alienda shuleni ambapo babake alifunza Kifaransa. Baadaye alienda shule ya mabweni katika eneo la Blida.


Je, wajua...?[hariri | hariri chanzo]


Wasifu Uliochaguliwa[hariri | hariri chanzo]

Wasifu Uliochaguliwa kwa Julai 2012[hariri | hariri chanzo]

Kofi Annan

Kofi Annan alikuwa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa 1996 - 2006. Alizaliwa 8 Aprili 1938 huko Kumasi, Ghana. Alipewa jina Kofi kuonyesha kuwa alizaliwa siku ya Ijumaa kuendana na utamaduni wa Ashanti. Jina Annan linamaanisha kuwa alikuwa ni mtoto wa nne kuzaliwa. Baada ya masomo ya uchumi alijiunga na huduma ya Umoja wa Mataifa mwaka 1962 katika WHO. 1974-1976 alifanya kazi Ghana halafu akarudi tena huduma ya UM. Akapanda ngazi kuwa Makamu wa Katibu Mkuu mhusika wa usalama aliwajibika kusimamia shughuli za wanajeshi walio chini ya UM.


kuchaguliwa picha kwa 2012[hariri | hariri chanzo]

kuchaguliwa picha kwa Julai 2012[hariri | hariri chanzo]

Nile sunset dar almanasir.JPG


Sunset katika Mto Nile kwa kisiwa cha Sherari, Dar al-Manas, kaskazini mwa Sudan.
(kupata bango)