Jimbo Katoliki la Zanzibar

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Kanisa kuu la Mt. Yosefu, Zanzibar.
Hii ni sehemu ya mfululizo kuhusu
Kanisa Katoliki
Imani

Umoja wa Mungu
Utatu (Baba, Mwana, Roho Mtakatifu)
Umwilisho Maisha ya Yesu
Msalaba Ufufuko Kupaa
Historia ya Wokovu Ufunuo
Biblia Mapokeo Ualimu Dogma
Neema Dhambi Wokovu Sakramenti
Watakatifu Bikira Maria

Muundo

Papa: Fransisko
Urika wa maaskofu Mitaguso mikuu
Kundi la Makardinali
Kanisa la Kilatini
Makanisa Katoliki ya Mashariki

Historia

Historia Ukristo
Ukatoliki Mlolongo wa Kitume
Sifa nne za Kanisa Utetezi Ekumeni
Maisha ya kiroho Amri Kumi Utawa
Sala Falsafa Teolojia
Muziki Sanaa Sayansi

Ibada

Liturujia Mwaka wa Kanisa
Ekaristi Liturujia ya Vipindi

Mapokeo ya liturujia

Liturujia ya Kilatini (Roma Liturujia ya Trento Milano Toledo Braga Lyon Canterbury)
Liturujia ya Armenia Liturujia ya Misri
Liturujia ya Ugiriki Liturujia ya Antiokia
Liturujia ya Mesopotamia

Jimbo Katoliki la Zanzibar (kwa Kilatini "Dioecesis Zanzibarensis") ni mojawapo kati ya majimbo 34 ya Kanisa Katoliki nchini Tanzania, likienea katika visiwa vya Unguja na Pemba vya Tanzania visiwani, jumla kilometa mraba 2,332.

Makao makuu yake ni katika mji wa Zanzibar na linahusiana na Jimbo kuu la Dar-es-Salaam.

Kanisa kuu limewekwa wakfu kwa heshima ya Mtakatifu Yosefu.

Askofu wa jimbo ni Augustine Ndeliakyama Shao, C.S.Sp.

Historia[hariri | hariri chanzo]

Ukristo ulianzishwa na wamisionari wa Shirika la Mt. Agostino kutoka Ureno walioongozana na Vasco da Gama mwaka 1499 hadi Zanzibar.

Huko walijenga konventi ya shirika lao ili kuhudumia kiroho Wakristo toka Ulaya tu.

Misheni ilipingwa na Waarabu Waislamu na kukoma mwaka 1698, kisiwa hicho kilipotekwa na Waarabu wa Oman.

Uinjilishaji ulianza upya katika sehemu ya pili ya karne ya 19 ambapo tangu mwaka 1860 Zanzibar ilikuwa makao makuu ya Vikarieti ya Kitume iliyoenea hata bara.

Jimbo liliundwa rasmi tarehe 28 Machi 1980 baada ya kujitegemea tangu 12 Desemba 1964 kama Apostolic Administration.

Takwimu[hariri | hariri chanzo]

Waumini ni 12,794 (2010) kati ya wakazi 1,221,000 (sawa na 1%), wengi wao wakiwa Waislamu.

Mapadri ni 20, ambao kati yao 18 ni wanajimbo na 2 ni watawa. Hivyo kwa wastani kila mmoja anahudumia waumini 639 katika parokia 7.

Mabruda jimboni ni 6, na masista 48.

Maaskofu[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu Kanisa Katoliki bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Jimbo Katoliki la Zanzibar kama historia yake au maelezo zaidi?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.