Hifadhi ya kisiwa cha Saanane

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Kisiwa cha Saanane (Saanane Island National Park) ni hifadhi ya taifa la Tanzania na ni hifadhi ndogo yenye eneo la kilomita za mraba 2.18, na iko umbali wa kilometa 2 kusini magharibi kutoka katikati ya jiji la Mwanza, katika Ghuba ya Ziwa Victoria nchini Tanzania.

Hifadhi hii ilianzishwa kama bustani ya kwanza ya wanyama nchini Tanzania mwaka 1964 ikawa hifadhi kamili mwaka 2013.

Lengo la kuanzishwa kwake ilikuwa kuhamasisha uhifadhi wa wanyama na kuelimisha jamii, pamoja na kutoa nafasi kwa wakazi wa Mwanza kupumzika.

Pundamilia katika hifadhi

Jina la hifadhi hii lilitokana na muanzilishi wa bustani aitwaye Saanane Chawandi. Kati ya mwaka 1964 na 1966 wanyama mbalimbali walihamishiwa katika kisiwa hiki.

Wanyama hao ni pamoja na mbogo, digidigi, tembo, pofu, pongo, swala pala, ngiri, pundamilia, kima, twiga, nungunungu, mamba n.k

Wanayama wakali kama faru na mbogo walifungiwa na wanyama wapole waliachwa huru.

Bustani hii iliachwa kuwa pori la akiba mwaka 1991.

Muonekano wa Ziwa Victoria katika kisiwa cha Saanane ni kivutio kikubwa. Vilevile muonekano wa Kisiwa cha Saanane uwapo Mwanza ni kivutio kingine kikubwa.

Hifadhi hii inafikika wakati wowote katika mwaka. Na unaweza kufika kwa kutumia boti ukitokea katika mji wa Mwanza.

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Mwanza bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Hifadhi ya kisiwa cha Saanane kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Tafadhali usiingize majina ya maafisa au viongozi wa sasa maana wanabadilika mno.