IPP Media

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

IPP Media ni kampuni ya magazeti, televisheni na redio nchini Tanzania.[1]

Kwa Kiswahili IPP inachapisha magazeti ya Nipashe, Alasiri, Komesha, Kasheshe na Lete Raha, na kwa Kiingereza kampuni hiyo inachapisha The Guardian,[2] Sunday Observer, Financial Times table na This Day.

IPP ina vituo vitatu vya televisheni, Independent Television (ITV) Channel 5 East Africa TV (5 EATV) na capital television , na vituo vya redio ni Radio One, East Africa FM na capital radio.

Pia, tovuti ya IPP, ippmedia.com, ni chanzo kikubwa cha habari kwa Kiswahili na kuhusu Tanzania kwenye mtandao.

Makao makuu ya IPP Media yako jijini Dar es Salaam. Mwenyekiti wa kampuni hii alikuwa Reginald Mengi.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu mambo ya uchumi bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu IPP Media kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.