Mkoa wa Unguja Mjini Magharibi
6°10′00″S 39°15′00″E / 6.1667°S 39.2500°E


Mkoa wa Unguja Mjini Magharibi ni kati ya mikoa 31 ya Tanzania. Uko Unguja ambacho ni kisiwa kikubwa cha Jamhuri ya Watu wa Zanzibar. Unapakana na mikoa yote miwili mingine ya kisiwa hicho: Mkoa wa Unguja Kusini na Mkoa wa Unguja Kaskazini mbali ya Bahari Hindi. Eneo la mkoa ni km² 230 ambako kuna jumla ya wakazi 893,169 kadiri ya sensa ya mwaka 2022 [1]. Walikuwa 593,678; Mjini 223,033 na Magharibi 370,645 katikasensa ya mwaka 2012[2]. Makao makuu ya mkoa yako Zanzibar. Sehemu ya jiji hilo, maarufu kama Mji Mkongwe, imeorodheshwa na UNESCO kama Urithi wa Dunia.
Msimbo wa posta ni namba 71000.
Mkoa huu una wilaya tatu ambazo ndizo Mjini, yaani Jiji la Zanzibar, Unguja Magharibi A na Unguja Magharibi B.
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]
Tazama pia
[hariri | hariri chanzo]Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]| Arusha | Dar es Salaam | Dodoma | Geita | Iringa | Kagera | Katavi | Kigoma | Kilimanjaro | Lindi | Manyara | Mara | Mbeya | Morogoro | Mtwara | Mwanza | Njombe | Pemba Kaskazini | Pemba Kusini | Pwani | Rukwa | Ruvuma | Shinyanga | Simiyu | Singida | Songwe | Tabora | Tanga | Unguja Kaskazini | Unguja Kusini | Unguja Mjini Magharibi | |
| Makala hii kuhusu maeneo ya Unguja bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Mkoa wa Unguja Mjini Magharibi kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. Tafadhali usiingize majina ya maafisa au viongozi wa sasa maana wanabadilika mno. |
