Nenda kwa yaliyomo

Kokain

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Kokeni)
Unga wa kokaini.
Mlin'ganyo wa kikemia wa cocaine.

Kokain (kutoka Kiingereza Cocaine, pia inajulikana kama coke), ni kisisimua-mwili au dawa ya kulevya inayotengenezwa kutokana na majani ya kituka cha koka kinachostawi katika milima ya Amerika Kusini. Umbo lake ni unga wa fuwele nyeupe.

Ilianza kutumiwa kama dawa ya kutuliza maumivu, halafu ikatambuliwa kama dawa ya kulevya na hivyo kusambaa kimataifa.

Kwa kawaida hunuswa, huvutwa kama moshi, au kama suluhisho hudungwa katika mshipa ya damu.

Matumizi ya kiganga

[hariri | hariri chanzo]

Tiba hutumia kokain kama dawa ya kutuliza maumivu hasa wakati wa upasuaji mdomoni na puani.

Dawa ya kulevya

[hariri | hariri chanzo]

Kiasili wenyeji wa Amerika Kusini walitafuna majani ya koka jinsi watu wa Afrika ya Mashariki na Arabia hutafuna majani ya miraa, kwa jina lingine mirungi.

Kiasi cha dawa kinachopatikana katika majani hakileti ulevi bali hutuliza njaa na kuondoa uchovu.

Tangu mwaka 1860 wanakemia wameweza kuondoa dawa tupu kutoka majani kama unga. Kutokana na matumizi ya tiba watu walianza kuonja dawa na kutambua uwezo wake wa kusababisha ndoto na hali ya kujisikia raha. Ilionekana baadaye ya kwamba kokain ina tabia kama madawa mengine ya kulevya ya kuwa watu huzoea haraka kiasi cha kutawaliwa na dawa: hawawezi kuiacha (uraibu).

Upande wa akili madhara yake yanaweza kujumuisha kukosa mawasiliano katika ubongo au fadhaa. Upande wa mwili dalili zake ni pamoja na kiwango kikubwa cha kasi ya moyo na jasho. Matumizi makubwa ya dozi yanaweza kusababisha shinikizo la damu la juu sana au joto la mwili.

Biashara

[hariri | hariri chanzo]

Siku hizi sehemu kubwa ya kokain hutegenezwa kwa matumizi ya dawa ya kulevya. Nje ya masharti ya tiba matumizi yake ni marufuku, lakini watu hupenda ndoto wanazopata kutokana na matumizi yake.

Mara wakitawaliwa na dawa huona haja ya kurudiarudia matumizi yake. Kwa sababu hiyo biashara ya kokain inazalisha pesa nyingi hata kama ni marufuku.

Majani ya koka huvunwa hasa katika nchi za Kolombia, Peru na Bolivia. Maabara kubwa za siri za kuondoa dawa ya kokain tupu ziko hasa Kolombia.

Mabwana wa biashara hii ni matajiri wakitumia wanamgambo wanaolinda eneo la maabara dhidi ya polisi. Kiasi cha pesa inayopatikana kimetosha mara kwa mara kuhonga wanasiasa na maafisa wa juu serikalini na hivyo kupata nafasi ya kuendesha maabara pamoja na biashara inayotumia ndege ndogo zinazopeleka kokain nje, ama moja kwa moja hadi Marekani au hadi visiwa vya Karibi ambako hufikishwa kwenye meli kwa biashara ya kimataifa.

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
Wikiquote ina mkusanyiko wa dondoo kuhusu:
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Simple English Wiktionary
Simple English Wiktionary
Wikamusi ya Kiswahili ina maelezo na tafsiri ya maana ya neno:
Makala hii kuhusu mambo ya kemia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Kokain kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.