Nenda kwa yaliyomo

Isimila

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Historia ya Tanzania
Coat of Arms of Tanzania
This article is part of a series
Uendo
Historia ya Zanzibar
Afrika Mashariki 1800-1845
Ukoloni
Afrika ya Mashariki ya Kijerumani
Mkataba wa Zanzibar-Helgoland
Mkwawa
Vita vya Maji Maji
Vita vikuu vya kwanza Afrika Mashariki
Tanganyika
Mapambano ya uhuru Tanganyika
Uhuru
Uhuru wa Tanganyika
Mapinduzi ya Zanzibar
Muungano wa Tanganyika na Zanzibar
Julius Nyerere
Ujamaa
Tamko la Arusha
Vita vya Kagera
Ali Hassan Mwinyi
Benjamin Mkapa
Jakaya Kikwete
John Magufuli
Samia Suluhu Hassan

Tanzania Portal

Isimila ni eneo la kihistoria lililopo katika kijiji cha Ugwachanya, kata ya Mseke, mkoani Iringa nchini Tanzania, kilomita 20 kutoka Iringa mjini karibu na barabara kuu ya A 104 kuelekea Mbeya.

Njia ya kuingia si rahisi kuikuta: ukitokea Iringa iko kabla ya kufikia Tanangozi, upande wa kushoto.

Eneo hili ni kivutio kimojawapo kinachoupamba mkoa wa Iringa.

Bonde la Isimila lilikaliwa na watu tangu Zama za Mawe za Kale. Ni katika eneo hilo ndipo zana za mawe za kale na nguzo za asili za Isimila zilipogunduliwa tangu mwaka 1951.

Zana hizo zinasadikiwa kuwa zilikuwepo tangu miaka 260,000 kabla ya Kristo, umri uliopatikana kwa kupimwa mifupa ya kibinadamu iliyokutwa kati ya mawe yaliyochongwa kama zana[1].

Miongoni mwa zana zilizopo katika korongo la Isimila, ambalo lina mikondo miwili, ni pamoja na mikuki iliyotumika kwa ajili ya kujihami na pia mawe ya kombeo kwa ajili ya uwindaji. Korongo la pembeni lina mmomonyoko wa ardhi ulioacha nguzo za ajabu.

Pia vifaa kama nyundo zilizokuwa zikitumika kwa ajili ya kutengenezea zana nyingine na shoka zilizotumika kwa kazi ya kuvunja mifupa, nyembe na visu.

Pia ndani ya eneo hili mafuvu na mifupa mingi vimeonekana; kati yake ilipatikana mifupa ambayo ilifanana na ya twiga wa hivi sasa, ila tofauti ni kwamba, mifupa hiyo iliashiria kuwa twiga hao walikuwa na shingo fupi, ambapo pia kulikuwa na aina tofauti ya viboko.

Tazama pia

[hariri | hariri chanzo]
  1. F. Clark Howell et al.: Uranium-series Dating of Bone from the Isimila Prehistoric Site, Tanzania. In: Nature. Band 237, 1972, S. 51–52, doi:10.1038/237051a0, online hapa

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]