Mkoa wa Mbeya
Mkoa wa Mbeya |
|
Mahali pa Mkoa wa Mbeya katika Tanzania | |
Majiranukta: 2°45′S 32°45′E / 2.750°S 32.750°E | |
Nchi | Tanzania |
---|---|
Wilaya | 7 |
Mji mkuu | Mbeya |
Serikali | |
- Mkuu wa Mkoa | Juma Zuberi Homera |
Eneo | |
- Jumla | 35,954 km² |
Idadi ya wakazi (2022) | |
- Wakazi kwa ujumla | 2,343,754[1] |
Tovuti: http://www.mbeya.go.tz/ |
Mkoa wa Mbeya ni kati ya mikoa 31 ya Tanzania, ukipakana na Zambia na Malawi, halafu na mikoa ya Rukwa, Tabora, Singida na Iringa, mbali na mkoa mpya wa Songwe uliomegwa kutoka ule wa Mbeya upande wa magharibi mwaka 2016.
Una Postikodi namba 53000.
Kabla ya kugawiwa kulikuwa na wilaya 9 zifuatazo: Mbeya Mjini, Mbeya Vijijini, Rungwe, Kyela, Ileje, Mbozi, Chunya, Momba na Mbarali.
Tangu 2016 mkoa umekuwa na wilaya 7 za: Busokelo, Chunya, Kyela, Mbarali, Mbeya Mjini, Mbeya Vijijini na Rungwe.[2]
Kadiri ya sensa ya mwaka 2022 idadi ya wakazi ni 2,343,754 [3].
Jiografia
Kijiolojia mkoa wa Mbeya ni eneo la kukutana kwa mikono miwili ya Bonde la Ufa la Afrika ya Mashariki inayoendelea hapa katika ziwa Nyasa. Mkoa wa Mbeya inapakana pia na Ziwa Rukwa. Hasa milima yenye asili ya volkeno ya wilaya ya Rungwe imejaa maziwa ya kasoko.
Mito mikubwa ni Songwe na Kiwira. Chanzo cha mto Ruvuma kiko pia Mbeya katika tambarare ya Usangu.
Wilaya ya Rungwe ni eneo lenye mvua nyingi katika Tanzania, ila maeneo makubwa ya Wilaya ya Chunya ni makavu.[2].
Mkoa kwa ujumla ni mmojawapo kati ya mikoa yenye kilimo kizuri inayotoa mazao ya kulisha taifa Mbeya na Mbozi kahawa hupandwa. Rungwe pana chai nyingi, pamoja na Rungwe na Chimala hulimwa mpunga. Nyanda za juu kuna nafaka na viazi.
Wilaya ya Chunya ina madini mbalimbali hasa dhahabu. Wenyeji wa wilaya ya Chunya ni Wabungu na waishio huko zaidi ni Wanyiha.
Usafiri
Kituo cha Reli
Mbeya inahudumiwa na Kituo cha Reli cha Mbeya ambacho kiko karibu na A104 au kupitia reli ya TAZARA kutoka mjini, kwa wiki hupokea treni mbili za abiria.[4]
Barabara
Mbeya inaweza kufikiwa kwa barabara kwenye barabara kuu ya A-7 kutoka Dar es Salaam , Kuna barabara za lami ambazo zinaunganisha jiji la Mbeya na miji mingine kama Tukuyu kupitia Uyole, Tunduma kupitia barabara kuu ya TANZAM na Chunya hadi Tabora kupitia Isanga.
Mbeya ina idadi kubwa ya abiria wanaoelekea Lusaka/Malawi kutoka Bandari ya Dar es Salaam ambao mara nyingi husimama mjini kwa ajili ya malazi ya usiku au chakula.
Uwanja wa Ndege
Mbeya inaunganishwa na Tanzania nzima kwa njia ya ndege kupitia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Songwe ambao ulifunguliwa Desemba 2012. Ni moja kati ya viwanja vinne vikubwa vya ndege vilivyopo Tanzania. Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Songwe uko ndani ya mkoa wa Mbeya na sio katika mkoa mpya wa Songwe. Uwanja huo upo umbali wa kilomita 25 kutoka katikati ya Jiji la Mbeya na umbali wa kilomita 2-3 kutoka mpaka wa mikoa ya Mbeya na Songwe ambao ni mto Songwe.
Vivutio vya kitalii
-
Ziwa Ngosi ni ziwa la pili kwa ukubwa barani Afrika lililotokana na mlipuko wa volkeno. Linapatikana karibu na Tukuyu, mji mdogo katika Wilaya ya Rungwe, Mkoa wa Mbeya.
-
Daraja la Mungu la Kiwira
-
Maporomoko ya maji ya Mwalalo.
-
Maporomoko ya maji ya Kapologwe yapatikana Mbeya
Mbeya ni kati ya maeneo yanayopendeza kabisa ndani ya Tanzania ikiwa na sehemu za ziwa Nyasa, Mlima ya Mbeya, Mlima ya Rungwe, Uwanda wa juu wa Uporoto, Uwanda wa Usangu ingawa haukufikiwa bado na utalii.[2]
Mvua kwa kawaida huanza mwezi Oktoba na kumalizika mwezi Mei, ikifuatiwa na kipindi kikavu na baridi kati ya Juni na Septemba. Utalii wa kawaida sio mchangiaji mkubwa wa uchumi wa ndani na hakuna miezi inayoonekana kuwa na watalii wengi.
Mbeya ipo katika Bonde la Ufa na unachukuliwa kama Csb na mfumo wa Köppen-Geiger. Hali ya hewa ya baridi na milima katika mji huvutia hasa wenyeji kutoka sehemu zingine za nchi na wageni kwa ajili ya michezo na uvuvi. Serikali ya eneo hilo imeanza kujaribu kupanua utalii zaidi ya kutazama wanyama pori, na imewekeza katika kuzalisha ramani bora na kuendeleza kituo cha utalii cha ndani.[5]
Mkoa wa Mbeya una idadi ya vivutio vya kitalii ambavyo ni pamoja na:
- Ziwa Ngosi
- Ziwa Kisiba
- Hifadhi ya Taifa Kitulo
- Pori la Akiba Mpanga Kipengere
- Maporomoko ya maji (Kapologwe, Malamba, Kimani, Isabula)
- Vilele vya Mlima Mbeya, Mlima Loleza, Mlima Rungwe
- Safu za Milima ya Kipengere (Livingstone)
Mbeya pia ina maeneo mbalimbali ya michoro ya kwenye miamba na mapangoni. Maeneo mengi ya miamba bado hayajasajiliwa na idara ya Antiequits na kutoa kioo cha kuangalia katika tamaduni za jadi za jamii zinazozunguka.
Majimbo ya bunge
Wakati wa uchaguzi mkuu wa Tanzania mwaka 2015 mkoa huu ulikuwa na majimbo ya uchaguzi yafuatayo:
- Busokelo : mbunge ni Atupele Mwakibete (CCM)
- Ileje : mbunge ni Janeth Mwamben (CCM)
- Kyela : mbunge ni Ally Jumbe Mlaghila (CCM)
- Lupa : mbunge ni Masache Njelu Kasaka (CCM)
- Mbarali : mbunge ni Haroon Mullah Pirmohamed (CCM)
- Mbeya Mjini : mbunge ni Tulia Ackson Mwansasu (CCM)
- Mbeya Vijijini : mbunge ni Oran M. Njeza (CCM)
- Mbozi : mbunge ni George Mwenisongole (CCM)
- Momba : mbunge ni Condester Michael Sichalwe (CCM)
- Rungwe : mbunge ni Sauli Henry Amon (CCM)
- Songwe : mbunge ni Philipo Mulugo (CCM)
- Tunduma : mbunge ni Mwakajoka Frank (Chadema)
- Vwawa : mbunge ni Hasunga Ngailanga (CCM)
Watu mashuhuri
- Godfrey Mwakikagile, mwandishi.
- Joseph Mbilinyi "Mr.II Sugu"; mbunge wa zamani wa Mbeya Mjini; msanii aliye miongoni mwa waanzilishi wa hip hop ya Tanzania.
- Rayvanny, mwanamuziki kutoka Nzovwe.
- Christopher Richard Mwashinga, mwandishi na mshairi kutoka Igawilo.
- Izzo Bizness, msanii wa rap.
- Fadhy Mtanga, mwandishi, mshairi, mwanablogu na mpiga picha.
- Davis Mwamunyange, alikuwa Mkuu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania.
- Mark Mwandosya, mbunge wa zamani wa jimbo la Rungwe Mashariki aliyekuwa Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano.
- Harrison George Mwakyembe, msomi na waziri wa zamani wa michezo.
- Tulia Ackson, aliyekuwa Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali, na kwa sasa Spika wa Bunge.
- John Mwakangale, kiongozi wa TANU na mpigania uhuru.
- Robert Mboma, mstaafu wa CDF.
- Mary Machuche Mwanjelwa, mbunge wa Viti Maalum tangu mwaka 2010.
Tazama pia
Viungo vya nje
- Tovuti rasmi ya Mkuu wa Mkoa
- Tovuti ya habari mbeyayetu Archived 3 Januari 2017 at the Wayback Machine.
- Mbeya Region Socioeconomic Profile katika TZOnline Archived 7 Machi 2022 at the Wayback Machine. (Kiingereza)
Marejeo
- ↑ https://www.nbs.go.tz
- ↑ 2.0 2.1 2.2 Chalamila, Albert (2018). "Mpango Mkakati, 2018-2023" (PDF) (kwa Kiingereza). Mkoa wa Mbeya. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka (PDF) kutoka chanzo mnamo 2022-07-17.
{{cite web}}
:|archive-date=
/|archive-url=
timestamp mismatch; 2022-06-17 suggested (help) - ↑ https://www.nbs.go.tz
- ↑ "TANZAM JOURNEY | Railways Africa". web.archive.org. 2012-04-23. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2012-04-23. Iliwekwa mnamo 2024-08-28.
{{cite web}}
: CS1 maint: bot: original URL status unknown (link) - ↑ "Tourism and Wildlife | Mbeya Region". web.archive.org. 2016-02-08. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2016-02-08. Iliwekwa mnamo 2024-08-28.
{{cite web}}
: CS1 maint: bot: original URL status unknown (link)
Arusha | Dar es Salaam | Dodoma | Geita | Iringa | Kagera | Katavi | Kigoma | Kilimanjaro | Lindi | Manyara | Mara | Mbeya | Morogoro | Mtwara | Mwanza | Njombe | Pemba Kaskazini | Pemba Kusini | Pwani | Rukwa | Ruvuma | Shinyanga | Simiyu | Singida | Songwe | Tabora | Tanga | Unguja Kaskazini | Unguja Kusini | Unguja Mjini Magharibi |
Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Mbeya bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Mkoa wa Mbeya kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. Tafadhali usiingize majina ya maafisa au viongozi wa sasa maana wanabadilika mno. |