Nenda kwa yaliyomo

Uyole

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru


Bonde la Uyole
Bonde la Uyole is located in Tanzania
Bonde la Uyole
Bonde la Uyole

Mahali pa Uyole katika Tanzania

Majiranukta: 8°53′24″S 33°25′48″E / 8.89000°S 33.43000°E / -8.89000; 33.43000
Nchi Tanzania
Mkoa Mbeya
Wilaya Mbeya Mjini
Idadi ya wakazi
 - Wakazi kwa ujumla 11,543

Uyole ni moja ya vitongoji vya Mbeya Mjini katika Mkoa wa Mbeya, Tanzania. Uyole iko kando ya eneo la halmashauri ya Mbeya takriban km 10 kutoka kitovu cha mji mahali penye njiapanda ambako barabara kuu ya TANZAM inaachana na barabara ya kuelekea Tukuyu na Malawi. Kitovu cha Uyole kipo katika njiapanda hiyo, hivyo basi jina maarufu la Uyole hupendwa kuitwa njiapanda ya Ulaya kutokana na umaarufu wa shughuli za mji huo.

Uyole kwa sasa ina jumla ya kata 7 ambazo ni: Nsalaga, Itezi, Igawilo, Isyesye, Uyole, Iduda na Iganjo. Kwa sasa Uyole imepewa dhamana ya kuwa halmashauri ndani ya jiji la Mbeya kwa kuongezwa kata kadhaa za jiji hilo kama Ilemi na Ilomba.

Wakati wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ya Uyole tu ilikuwa na wakazi wapatao 11,543[1]. Wakazi wa Uyole kwa sasa wanakadiriwa kuwa zaidi ya 100,000 na kuifanya kuwa miongoni mwa maeneo yenye wakazi wengi jijini Mbeya.

Msimbo wa posta ni 53136.

Kuna huduma za kila aina kwa makazi ya kibinadamu kama ofisi, masoko, vituo vya uchukuzi na usafirishaji kama kituo cha reli cha TAZARA. Stendi ya mabasi ya Nanenane na vyuo mbalimbali kama Chuo cha Kilimo Uyole, Chuo cha Maendeleo ya Jamii Uyole na kadhalika.

Chuo cha Kilimo Uyole (Agricultural Research Institute -ARI- Uyole) kinafundisha wanafunzi na ni kitovu cha uchunguzi wa kisayansi wa mimea ya kilimo.

  1. "Sensa ya 2012, Mbeya - Mbeya MC" (PDF). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo (PDF) mnamo 2016-03-03. Iliwekwa mnamo 2017-03-14.
Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Mbeya bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Uyole kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Tafadhali usiingize majina ya maafisa au viongozi wa sasa maana wanabadilika mno.