Lubumbashi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Lubumbashi katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
Lumbumbashi mjini

Lubumbashi (zamani ilkuwa inaitwa Elisabethville au Elisabethstad) ni mji uliopewa heshima kama mji wa pili kwa ukubwa katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (mji mkuu wake Kinshasa, zamani iliitwa Zaire) vile vile ni kitovu cha kusini-mashariki mwa nchi. Mji huo una mgodi wa shaba unaochukuliwa kama kitumio cha mradi husika katika kuiletea neema mkoa wa Katanga (zamani uliitwa Shaba) mkoa, umepakana karibu na mpaka wa nchi ya Zambia. Idadi ya wakazi wa huko wapo takribani milioni 1.2 ila tu mji unasemekana kuwa una wanyama wakali mno.

Yaliyomo

[hariri] Jiografia

Lubumbashi uko kwenye kimo cha mita 1,000 juu ya usawa wa bahari. Mto Kafue umekutana na mpaka wa Zambia karibu kidogo na mji, mto huo umepitapita hadi kutokea sehemu za Zambia na kwenda kuungana na Mto Zambezi.

[hariri] Historia

Mji ulianzishwa mwaka 1909/1910 na Wabelgiji katika koloni ya Kongo ya Kibelgiji. Eneo la Katanga lina madini mengi na Wabelgiji walianzisha migodi ya madini katika eneo. Mahali pa Lumbumbashi walianzisha migodi pamoja na makazi ya wafanyakazi yaliyoitwa Elisabethville / Elisabethstaad kwa heshima ya Elisabeth wa Wittelsbach mke wa mfalme mteule Albert I wa Ubelgiji.

1910 reli ilifikia Elisabethville na kuunganisha mji na Afrika Kusini kupitia Zambia. Mji ukakua haraka pamoja na mahitaji ya migodi. 1954-55 chuo kikuu kikajengwa.

Wakati wa uhuru Elisabethville ilikuwa kitovu cha harakati ya kuunda dola la Katanga lililotengwa na Kongo kati ya 1960 hadi 1963 chini ya Moise Tshombe. Mji ulivamiwa na jeshi la Umoja wa Mataifa na kurudishwa chini ya serikali ya Kongo.

1966 mji ulibadilishwa jina na rais Mobutu Sese Seko na kupewa jina jipya la Lubumbashi kufuatana na mto katika eneo la mji.

[hariri] Uchumi na kilimo

[hariri] Viungo vya Nje