Jimbo Kuu la Dar-es-Salaam
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jimbo Kuu la Dar-es-Salaam (kwa Kilatini Archidioecesis Daressalaamensis) ni mojawapo kati ya majimbo 33 ya Kanisa Katoliki nchini Tanzania na kama hayo yote linafuata mapokeo ya Kiroma.
Chini yake kuna kanda ya Kanisa yenye majimbo yafuatayo: Zanzibar, Tanga, Morogoro, Mahenge, Dodoma na Kondoa.
Askofu mkuu wake ni kardinali Polycarp Pengo.
Yaliyomo |
Historia[hariri]
- 1887: Kuanzishwa kwa Apostolic Prefecture ya Dar-es-Salaam kutokana na Apostolic Vicariate ya Nairobi
- 1902: Kupandishwa cheo kuwa Apostolic Vicariate ya Dar-es-Salaam
- 1953: Kufanywa dayosisi
Uongozi[hariri]
- Maaskofu wa Dar-es-Salaam
- Polycarp Pengo (TANGU 1992)
- Laurean Rugambwa (1968 – 1992)
- Edgar Aristide Maranta OFMCap (1953 – 1968)
- Vicar Apostolic wa Dar-es-Salaam
- Edgar Aristide Maranta OFMCap (1930 – 1953)
- Joseph Gabriel Zelger OFMCap (1923 – 1929)
- Thomas Spreiter OSB (1906 – 1920)
- Cassian Spiß OSB (1902 – 1905)
- Prefect Apostolic wa Dar-es-Salaam
- Padri Maurus Hartmann OSB (1894 – 1902)
- Padri Bonifatius Fleschutz OSB (1887 – 1891)
Takwimu[hariri]
Eneo la jimbo lina kilometa mraba 40,000 hivi, ambapo kati ya wakazi 5,003,000 (2006) Wakatoliki ni 1,490,000 (sawa na 29.8%).