Polycarp Pengo

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta

Polycarp Pengo ni kardinali wa pili kutoka Tanzania.

Maisha [hariri]

Alizaliwa Mwazye (mkoa wa Rukwa) tarehe 5 Agosti 1944.

Alipewa upadri mwaka 1971 na askofu Charles Msakila, akasoma teolojia ya maadili huko Roma akijitwalia digrii yaudaktari mwaka 1977.

Kisha kufundisha somo hilo kwenye seminari kuu ya Kipalapala (mkoa wa Tabora) kwa muda mfupi, alichaguliwa kuwa gombera wa seminari kuu ya Segerea hadi 1983.

Aliteuliwa askofu wa Nachingwea tarehe 11 Novemba 1983, akapewa daraja takatifu hiyo na Papa Yohane Paulo II tarehe 6 Januari 1984. Tarehe 17 Oktoba 1986 alihamishiwa jimbo jipya la Tunduru-Masasi.

Tarehe 22 Januari 1990 alifanywa askofu mwandamizi wa Dar-es-Salaam na mwaka 1992, kardinali Laurean Rugambwa alipojiuzulu, akawa askofu mkuu.

Aliteuliwa na Yohane Paulo II kuwa kardinali tarehe 21 Februari 1998, akikabidhiwa parokia ya Nostra Signora de La Salette mjini Roma.

Pamoja na majukumu mbalimbali katika idara za Papa, tangu mwaka 2007 ni Mwenyekiti wa Umoja wa Mabaraza ya Maaskofu Katoliki ya Afrika na Madagaska.

Viungo vya nje [hariri]