Jimbo Katoliki la Sumbawanga

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta

Jimbo Katoliki la Sumbawanga (kwa Kilatini Dioecesis Sumbavangensis) ni mojawapo kati ya majimbo 33 ya Kanisa Katoliki nchini Tanzania, na kama hayo yote linafuata mapokeo ya Kiroma.

Kanisa kuu liko mjini Sumbawanga, katika mkoa wa Rukwa.

Lilianzishwa tarehe 10 Mei 1946 na linahusiana na Jimbo Kuu la Tabora.

Askofu wa sasa ni Damian Kyaruzi.

Takwimu[hariri | hariri chanzo]

Eneo lake lote ni kama kilometa mraba 28.654, ambamo wamo wakazi 928.941. Kati yao Wakatoliki ni 607.143 (2004) yaani asilimia 65.4.

Waamini hawa wanahudumiwa na mapadri 53, ambao kati yao 49 ni wanajimbo na 4 watawa. Hivyo kwa wastani kila mmojawao anahudumia waamini 11.455.

Parokia ziko 22.

Jimbo lina mabruda 71 na masista 208.

Mlolongo wa maaskofu[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]