Seminari

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Seminari kuu)
Misa katika seminari kuu ya Asidonia-Jerez.

Seminari ni muundo wa malezi unaotoa mafunzo ya dini, hususan Ukristo, yakiwa pengine pamoja na elimu dunia.

Seminari kuu, au vyuo vya teolojia, ni muundo wa malezi ya juu kwa watu wanaolenga moja kwa moja upadri au huduma nyingine ya uongozi katika Kanisa.

Tofauti na hiyo, seminari ndogo inalea vijana kuanzia baadhi ya madarasa ya shule ya msingi hadi vidato vya sekondari.

Neno linatokana na Kilatini: seminarium ina maana ya kitalu, mfano uliotumiwa na Mtaguso wa Trento katika hati Cum adolescentium aetas ambayo ilianzisha seminari za kwanza za kisasa.[1]

Baada ya muundo huo kuenea katika Kanisa Katoliki, hata madhehebu mengine na hatimaye dini nyingine vimeanza kutumia mbinu hiyo.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. XXIII Session, Council of Trent, ch. XVIII. Retrieved from J. Waterworth, mhariri (1848). The Canons and Decrees of the Sacred and Oecumenical Council of Trent. London: Dolman. ku. 170–92. Iliwekwa mnamo June 16, 2009.  Check date values in: |accessdate= (help)

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu mambo ya dini bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu mada hii kama historia yake au uenezi wake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.