Nenda kwa yaliyomo

Yohane wa Kapestrano

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mt. Yohane wa Capistrano
Picha yake huko Ilok, Croatia, alipozikwa.

Yohane wa Kapestrano (Capestrano, wilaya ya L'Aquila, Italia, 24 Juni 1386 - Ilok, katika Korasia ya leo, 23 Oktoba 1456) alikuwa padri wa Kanisa Katoliki na mtawa wa shirika la Ndugu Wadogo ambalo alichangia kulirekebisha kufuatana na nia za mwanzilishi, Fransisko wa Asizi.

Alitangazwa kuwa mtakatifu na Papa Aleksanda VIII tarehe 16 Oktoba 1690.

Anaheshimiwa hasa kama msimamizi wa mapadri wanaohudumia wanajeshi.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe ya kifo chake[1].

Maisha[hariri | hariri chanzo]

Mtoto wa baba Mjerumani na mama Mwitalia, alisomea Perugia alipopata digrii za sheria za nchi na za Kanisa.

Baada ya kupata umaarufu kama wakili, alichaguliwa kuwa gavana wa mji huo hadi ulipotekwa na ukoo wa Malatesta ambao walimfunga.

Gerezani aliongoka, akakubaliwa ndoa yake itangazwe ni batili akaingia utawani kwa Wafransisko.

Kama padri alihubiri katika sehemu kubwa ya Ulaya, hasa upande wa Kaskazini na Mashariki, na kwa namna ya pekee Hungaria.

Lengo la hotuba na kazi zake zote lilikuwa kurekebisha maisha ya Wakatoliki, kupambana na uzushi (hasa Fraticelli, Wajesuati na Wahusi) pamoja na kuwafanya Wayahudi wamuamini Yesu Kristo.

Mwaka 1456 aliagizwa na Papa, akahubiri pamoja na ndugu wengine Vita vitakatifu dhidi ya Waturuki waliovamia Ulaya Kusini Mashariki.

Akizunguka Ulaya Mashariki alifaulu kukusanya maelfu ya waamini aliowaongoza kulinda mji wa Belgrad (Serbia) mwezi Julai mwaka huo: jeshi la Uturuki lilikimbia na sultani mwenyewe (Mehmed II) alijeruhiwa.

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.