Wikipedia ya Kiitalia

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Wikipedia ya Kiitalia

Wikipedia ya Kiitalia (Kiitalia: Wikipedia in italiano) ni toleo la kamusi elezo ya Wikipedia kwa lugha ya Kiitalia. Toleo hili lilianzishwa mnamo mwezi wa Januari katika mwaka wa 2002 na ina makala zaidi ya 527,000 na watu waliojisajiri ni zaidi ya 338,000 kwa tar. 5 Januari 2009[1].

Mnamo mwezi wa Agosti 2005, Wikipedia ya Kiitalia imeipita toleo la Wikipedia ya Kihispania na Kireno, na kuifanya iwe Wikipedia ya 8 kwa ukubwa wa hesabu ya makala. Sababu za msingi zilizopelekea Wikipedia hii kuwa kubwa ni baada ya kuruka idadi ya makala kutoka 56,000 hadi 64,000. Ambazo zote zilifanywa na maroboti ambao walitengeneza makala za mbegu zaidi ya 8,000 kuhusu miji na maeneo ya Hispania.[2][3]

Mnamo tar. 8 Septemba 2005, Wikipedia ya Kiitalia imeipita Wikipedia ya Kiholanzi na baada ya siku moja, mnamo 9 Septemba, ikapita makala 100,000. Mnamo tar. 11 Septemba, imeipita Wikipedia ya Kiswidi, na kuifanya iwe toleo la Wikipedia ya tano kwa ukubwa. Tena, maboti yakafanya michango mizito kwa kuikuza Wikipedia hii. Kwa mfano, maboti yametunga zaidi ya makala 35,000 kuhusu manispaa za Ufaransa.[4] Hata hivyo, ilikuja kupitwa na Wikipedia ya Kipoland mnamo tar. 23 Septemba 2005.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. Italian Wikipedia. Speciale:Statistics. Iliwekwa mnamo 2009-01-05.
  2. Italian Wikipedia. Wikipedia:Ultime_notizie. Iliwekwa mnamo 2008-02-23.
  3. Italian Wikipedia. Progetto:Geografia/Antropica/Comuni_spagnoli. Jalada kutoka ya awali juu ya 2006-09-13. Iliwekwa mnamo 2008-02-23.
  4. Italian Wikipedia. Progetto:Comuni_della_Francia. Jalada kutoka ya awali juu ya 2006-09-13. Iliwekwa mnamo 2008-02-23.

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Wikipedia
Wikipedia
Wikipedia ya Kiitalia ni toleo la Wikipedia, kamusi elezo huru
Makala hii kuhusu mambo ya elimu bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Wikipedia ya Kiitalia kama historia yake, uenezi au maendeleo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.