Nenda kwa yaliyomo

Wikipedia ya Kiholanzi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Wikipedia ya Kiholanzi
The Dutch Wikipedia in Mei 2007

Wikipedia ya Kiholanzi (Kiholanzi: Nederlandse Wikipedia) ni toleo la kamusi elezo ya Wikipedia kwa lugha ya Kiholanzi. Hii ilianzishwa mnamo tar. 19 Juni katika mwaka wa 2001, na ikafikisha makala 100,000 kunako tar. 14 Oktoba ya mwaka wa 2005.

Kwa muda mfupi ikawa imeipita Wikipedia ya Kipoland ikiwa kama Wikipedia ya sita kwa ukubwa, lakini baadaye ikarudi nyuma na kuwa sehemu ya nane kwa ukubwa. Mnamo tar. 24 Januari 2006, idadi ya makala imeongezeka na kuwa 125,000. Mnamo tar. 1 Machi 2006, ikaipiku Wikipedia ya Kiswidi na Kiitalia, yaani, ilikuwa kwa siku moja tu na kurudi tena katika sehemu yake ya sita.

Mnamo tar. 19 Machi 2006, takriban makala 150,000 ziliongezeka na baadaye ikawa na makala nyingine zilizoongezeka na kufikia 200,000 hiyo ilikuwa kunako tar. 24 Mei 2006. Mradi huu ulifikia makala 300,000 mnamo tar. 28 Mei ya mwaka wa 2007. Na kwa tar. 10 Januari ya mwaka wa 2008, Wikipedia hii imetunga zaidi ya makala 400,000 articles. Lengo la kufikisha makala 500,000 lilifikiwa mnamo tar. 30 Novemba katika huohuo wa 2008.[1]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. 500.000e artikel (website in Dutch language), retrieved 7 Desemba 2008

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Wikipedia
Wikipedia
Wikipedia ya Kiholanzi ni toleo la Wikipedia, kamusi elezo huru
Makala hii kuhusu mambo ya elimu bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Wikipedia ya Kiholanzi kama historia yake, uenezi au maendeleo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.