Wikipedia ya Kiafrikaans (Kiafrikaans: Afrikaanse Wikipedia) ni toleo la kamusi elezo huru ya Wikipedia kwa lugha ya Kiafrikaans. Mradi huu ulianzishwa mnamo tar. 16 Novemba2001, na ilikuwa Wikipedia ya 11 kuanzishwa.[1] Na kwa tar. 13 Mei2009, toleo hili limepita makala zaidi ya 12, 000[2] na kulifanya liwe tole la 79 la Wikipedia kwa ukubwa wa hesabu ya wingi makala. Lakini kwa sasa ni toleo la 79 kwa ukubwa baada ya Wikipedia ya Kiswahili. Mbali na Waafrika Kusini, Wikipedia pia uhaririwa na watu wa kutoka kule Uholanzi, Ubelgiji, Namibia, Ujerumani na baadhi yao kutoka nchini za Skandinavia.[3]
Awali lilikuwa toleo kubwa la Wikipedia katika lugha za Kiafrika, na pia lilikuwa toleo la kwanza la Wikipedia ya lugha za Kiafrika kupita makala zaidi 10,000[4].