Nenda kwa yaliyomo

Maisha na Nyakati za Abdulwahid Sykes

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Maisha na Nyakati za Abdulwahid Sykes
Toleo la 2002
MwandishiMohamed Said
MfasiriAli Salum Mkangwa
NchiTanzania
LughaKiswahili
SubjectMambo ya Uhuru
AinaUhuru wa kisiasa, harakati za uhuru
Kimechapishwa2002,2012
MchapishajiPhoenix Publishers, Nairobi
Kurasa416
ISBN9966-47-169-3 (Toleo la Kwanza)
Website"Tovuti Rasmi ya Mohamed Said"
Historia ya Tanzania
Coat of Arms of Tanzania
This article is part of a series
Uendo
Historia ya Zanzibar
Afrika Mashariki 1800-1845
Ukoloni
Afrika ya Mashariki ya Kijerumani
Mkataba wa Zanzibar-Helgoland
Mkwawa
Vita vya Maji Maji
Vita vikuu vya kwanza Afrika Mashariki
Tanganyika
Mapambano ya uhuru Tanganyika
Uhuru
Uhuru wa Tanganyika
Mapinduzi ya Zanzibar
Muungano wa Tanganyika na Zanzibar
Julius Nyerere
Ujamaa
Tamko la Arusha
Vita vya Kagera
Ali Hassan Mwinyi
Benjamin Mkapa
Jakaya Kikwete
John Magufuli
Samia Suluhu Hassan

Tanzania Portal

Maisha na Nyakati za Abdulwahid Sykes ni jina la kitabu kinachoelezea maisha na harakati zilizokuwa zinafanywa na hayati Abdulwahid Sykes katika kupigania uhuru wa Tanganyika kutoka mikononi mwa wakoloni katika miaka ya 1950. Harakati ambazo katika historia ya Tanzania leo hii haijawekwa wala kugusiwa. Kitabu kinaelezea historia iliyofichwa kuhusu Waislamu dhidi ya ukoloni wa Waingereza katika Tanganyika.

Muhtasari wa kitabu

[hariri | hariri chanzo]

Wakati wa utawala wa Julius Nyerere kama rais wa Tanzania mambo matatu yalikuwa mwiko kuelezea: kuwa historia ya kudai uhuru wa Tanganyika ilianza kabla yake; kuwa Waislamu ndio waliokuwa katika mstari wa mbele katika harakati za kupambana na wakoloni; kuwa kutokana na historia ya kudai uhuru Waislamu walikuwa na kinyongo na serikali kwa kutothamini mchango wao na kutotekeleza ahadi iliyowekwa wakati wa kudai uhuru.

Mwandishi ameelezea na kufanya utafiti wa kina katika masuala hayo yote. Kupitia maisha ya marehemu Abdulwahid Sykes na kumbukumbu za baba yake Kleist Sykes, mwandishi anamfunulia msomaji majina na juhudi za wazalendo wa mwanzo waliopambana na wakoloni na kumkutanisha na waasisi na viongozi wa kisiasa katika African Association mnamo miaka ya 1920.

Hali kadhalika kitabu kinaelezea michango chanya na adimu kuhusu wazalendo na viongozi vijana walioanzisha TANU mwaka 1954 kudai uhuru wa Tanganyika chini ya uongozi wa Julius Nyerere. Katika kufanya hivi, kitabu kimewatoa hofu wale waliokuwa wakidhani ya kwamba kuandika historia inayopingana na "historia rasmi" ni kukosa uzalendo na mapenzi kwa nchi yao.

Tazama pia

[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
Makala hii kuhusu kitabu fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Maisha na Nyakati za Abdulwahid Sykes kama Mwandishi wake, hadithi au matoleo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.