Biashara ya ng'ambo ya Sahara : Tofauti kati ya masahihisho

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Content deleted Content added
No edit summary
Mstari 1: Mstari 1:
[[Image:Oasis-Bilma.jpg|thumb|[[Oasisi]] ya [[Bilma]] mjini kaskazinimashariki mwa [[Niger]], kukiwa na mharara wa [[Kaouar]] kwa nyuma]]
[[Image:Oasis-Bilma.jpg|thumb|[[Oasisi]] ya [[Bilma]] mjini kaskazinimashariki mwa [[Niger]], kukiwa na mharara wa [[Kaouar]] kwa nyuma]]
'''Biashara ya ng'ambo ya Sahara''' (vilevile '''Biashara ya Masafa Marefu ya Afrika ya Magharibi''') ilikuwa biashara iliyohusisha [[Afrika ya Magharibi]] na [[Afrika ya Kaskazini]] kupitia [[jangwa la Sahara]]. Biashara hii ni mfano mzuri wa biashara za kanda au masafa marefu ambayo yaliyoongozwa katika upande wa Afrika Magharibi.
'''Biashara ya ng'ambo ya Sahara''' (vilevile '''Biashara ya Masafa Marefu ya Afrika ya Magharibi''') ilikuwa [[biashara]] iliyohusisha [[Afrika ya Magharibi]] na [[Afrika ya Kaskazini]] kupitia [[jangwa la Sahara]].
Biashara hiyo ni mfano mzuri wa biashara za kanda au [[masafa marefu]] ambayo yaliongozwa katika upande wa Afrika Magharibi.
Biashara hii ilianza mnamo [[karne ya 4]] na iliendelea zaidi hadi katika [[karne ya 7]] ambapo ilianguka mazima. Biashara ilikuwa na matokeo kadha wa kadha katika historia ya Afrika Magharibi na Afrika kwa ujumla.
Biashara hiyo ilianza mnamo [[karne ya 4]] na iliendelea zaidi hadi katika [[karne ya 17]] ambapo ilianguka mazima.

Biashara ilikuwa na matokeo kadha wa kadha katika [[historia ya Afrika Magharibi]] na [[Historia ya Afrika|ya Afrika]] kwa ujumla.

==Historia==
==Historia==
==Washiriki==
==Washiriki==
Washirika wakubwa wa biashara hii walikuwa watu kutoka Mataifa ya Kimagharibi ya Sudani, Ghana, Mali na Songhai na baadhi ya watu kutoka mjini Kaskazini mwa Afrika.
Washirika wakubwa wa biashara hii walikuwa watu kutoka Mataifa ya Kimagharibi ya Sudani, [[Ghana]], [[Mali]] na [[Songhai]] na baadhi ya watu kutoka mjini Kaskazini mwa Afrika.
===Kutoka Afrika Magharibi===
===Kutoka Afrika Magharibi===
Ilihusisha kikundi cha Wasoninke, Wamandika, Wayoruba, Wafulani, Wahausa, na wengineo wengi.
Ilihusisha kikundi cha [[Wasoninke]], [[Wamandika]], [[Wayoruba]], [[Wafulani]], [[Wahausa]] na wengineo wengi.
===Kutoka Afrika Kaskazini===
===Kutoka Afrika Kaskazini===
Ilihusisha kikundi cha Waarabu, Waberba, Watuareki na wengine wengi.
Ilihusisha kikundi cha [[Waarabu]], [[Waberberi]], Watuareki na wengine wengi.

==Bidhaa au vitu vilivyokuwa vinauzwa==
==Bidhaa au vitu vilivyokuwa vinauzwa==
Bidhaa zilizokuwa zinauzwa ni mchanganyiko, lakini vilevile mauzo yaliendana na kanda. Mafano:
[[Bidhaa]] zilizokuwa zinauzwa ni mchanganyiko, lakini vilevile mauzo yaliendana na kanda. Mifano:
===Kutoka Afrika Magharibi===
===Kutoka Afrika Magharibi===
Kutoka ndanindani kabisa ya misitu ya Afrika Magharibi, bidhaa zilikuwa dhahabu, fedha, ngozi za wanyama, pembe za ndovu, nta ya nyuki, asali and vitu vingine vya thamani vilivyoweza kubebeka.
Kutoka ndanindani kabisa ya [[misitu]] ya Afrika Magharibi, bidhaa zilikuwa [[dhahabu]], [[fedha]], [[ngozi]] za [[wanyama]], [[pembe za ndovu]], [[nta]] ya [[nyuki]], [[asali]] and vitu vingine vya thamani vilivyoweza kubebwa.
===Kutoka Afrika Kaskazini===
===Kutoka Afrika Kaskazini===
Kutoka Kaskazini, Waberba na Waarabu walileta bidhaa ndogondogo kwa mfano shanga, miwani, silaha na vingine vingi. Kwa upande wa jangwa la Sahara chumvi ilikuwa inapatikana kutoka Taghaza, Fez ba Bilima. Aina kuu ya usafiri wakati wa biashara hii ilikuwa punda, farasi na wakati mwingine walitembea kwa miguu. Lakini baadaye katika karne ya 7, ngamia aliletwa na Waarabu ambao waliwasili wakitokea [[Mashariki ya Kati]] na kuanza kutumika kama chombo kikuu cha usafiri kupitia Biashara ya Sahara.
Kutoka Kaskazini, Waberberi na Waarabu walileta bidhaa ndogondogo kwa mfano shanga, [[miwani]], [[silaha]] na vingine vingi. Kwa upande wa [[jangwa la Sahara]] [[chumvi]] ilikuwa inapatikana kutoka [[Taghaza]], [[Fez]] na [[Bilima]]. Aina kuu za [[usafiri]] wakati wa biashara hii ilikuwa [[punda]], [[farasi]] na wakati mwingine walitembea kwa miguu. Lakini baadaye katika karne ya 7, [[ngamia]] waliletwa na Waarabu ambao waliwasili wakitokea [[Mashariki ya Kati]] na kuanza kutumika kama chombo kikuu cha usafiri kupitia Sahara.

==Muundo wa biashara==
==Muundo wa biashara==
Biashara ilipangwa kwa mtindo misafara kama msururu ambayo ilianza kutoka kila upande wa Magharibi na Kaskazini mwa Afrika kupitia jangwa la Sahara. Misafara hiyo ilikuwa kama ifuatavyo:
Biashara ilipangwa kwa mtindo wa misafara kama [[msururu]] ambayo ilianza kutoka kila upande wa Magharibi na Kaskazini mwa Afrika kupitia jangwa la Sahara. Misafara hiyo ilikuwa kama ifuatavyo:
===(a) Msafara wa Magharibi===
===(a) Msafara wa Magharibi===
Msafara ulianza kutoka [[Sijilmasa]] na [[Fez]] huko nchini [[Morocco]]. Halafu unapitia [[Taghaza]], [[Taoden]], [[Watala]], [[Audaghost]], [[Kumbi Saleh]] hadi [[Timbuktu]].
Msafara ulianza kutoka [[Sijilmasa]] na [[Fez]] huko nchini [[Morocco]]. Halafu ukapitia [[Taghaza]], [[Taoden]], [[Watala]], [[Audaghost]], [[Kumbi Saleh]] hadi [[Timbuktu]].
===(b) Msafara wa Kati===
===(b) Msafara wa Kati===
Msafara ulianza kutoka [[Tunis]] wakapitia [[Ghat]], [[Kano]] kisha ukaenda zake na kupitia jangwani hadi [[Gao]] na mwisho kabisa [[Hausa]].
Msafara ulianza kutoka [[Tunis]] wakapitia [[Ghat]], [[Kano]] kisha ukaenda zake na kupitia jangwani hadi [[Gao]] na mwisho kabisa [[Hausa]].
===(c) Msafara wa Mashariki===
===(c) Msafara wa Mashariki===
Msafara huu ulianzia mjini [[Tripoli]] na ukaenda zake ha [[Marzul]] na mwisho kabisa ukamalizikia msafara huu huko mjini [[Bilima]].
Msafara huu ulianzia mjini [[Tripoli]] ukaenda zake hadi [[Marzul]] na mwisho kabisa ukamalizikia mjini [[Bilima]].

==Sababu zilizopelekea kukua kwa biashara==
==Sababu zilizopelekea kukua kwa biashara==
[[Image:Caravane hoggar1.jpg|thumb|Msafara wa ngamia wa siku hizi karibu na [[Milima ya Ahaggar]] katikati ya jangwa la Sahara, 2006]]
[[Image:Caravane hoggar1.jpg|thumb|Msafara wa ngamia wa siku hizi karibu na [[Milima ya Ahaggar]] katikati ya jangwa la Sahara, [[2006]].]]
Ukuaji na uendeleaji wa Biashara ya Ng'ambo ya Sahara iliathiriwa na mambo kadha wa kadha. Miongoni mwa sababu hizo ni pamoja na:
Ukuaji na uendeleaji wa Biashara ya Ng'ambo ya Sahara iliathiriwa na mambo kadha wa kadha. Miongoni mwa sababu hizo ni:
;A) '''Siasa Imara'''
;A) '''Siasa Imara'''
Nchi za Magharibi na Kaskazii hali ilikuwa shwari kabisa hakuna vita wala nini. Hili lilitoa chumba cha ukuaji wa biashara ya ng'ambo.
Katika nchi za Magharibi na Kaskazii hali ilikuwa [[shwari]] kabisa, hakukuwa na [[vita]] wala nini. Hili lilitoa chumba cha ukuaji wa biashara ya ng'ambo.
;B) '''Eneo la Kijiografia'''
;B) '''Eneo la Kijiografia'''
Mahali penyewe wanawezesha maendeleo ya kibiashara. Hili lilitokana na ukweli ni kwamba Magharibi na Kaskazini mwa Afrika zimepakana mno kupitia jangwa la Sahara.
Mahali penyewe panawezesha [[maendeleo]] ya kibiashara. Hili lilitokana na [[ukweli]] ni kwamba Magharibi na Kaskazini mwa Afrika zimepakana mno kupitia jangwa la Sahara.
;C) '''Upatikanaji wa bidhaa'''
;C) '''Upatikanaji wa bidhaa'''
Upatikanaji wa bidhaa huko Magharibi na Kaskazini mwa Afrika kulipelekea kukua kwa biashara ya ng'ambo.
Upatikanaji wa bidhaa huko Magharibi na Kaskazini mwa Afrika kulipelekea kukua kwa biashara ya ng'ambo.

;D) '''Utambulishaji wa ngamia kama zana ya kusarishia'''
;D) '''Utambulishaji wa ngamia kama zana ya kusarishia'''
Ngamia alitambulishwa na Waarabu kama zana kuu ya kusafirishia kupitia jangwa la Sahara katika karne ya 7. Hili lilirahisha shughuli za usafirishaji kupitia jangwani hivyo basi kupelekea ongezeko la ukuaji wa biashara hii.
Ngamia alitambulishwa na Waarabu kama zana kuu ya kusafirishia kupitia jangwa la Sahara katika karne ya 7. Hili lilirahisha shughuli za usafirishaji kupitia jangwani hivyo basi kupelekea ongezeko la ukuaji wa biashara hii.
;E) '''Uwepo wa chemchemi jangwani'''
;E) '''Uwepo wa chemchemi jangwani'''
Haya ni maeneo ya jangwa yenye vyanzo vya maji. Uwepo wa maeneo haya yenye maji umepelekea upatikanaji wa maji hayo kwa ajili ya ngamia na wafanyabiashara hivyo kuzidi kuchochea maendeleo ya ukuaji wa kibiashara.
Haya ni maeneo ya jangwa yenye vyanzo vya [[maji]]. Uwepo wa maeneo haya yenye maji umepelekea upatikanaji wa maji hayo kwa ajili ya ngamia na [[wafanyabiashara]], hivyo kuzidi kuchochea maendeleo ya ukuaji wa kibiashara.
;F) '''Ujio wa Waarabu'''
;F) '''Ujio wa Waarabu'''
Ujio wa Waarabu katika Afrika ya Kaskazini hasa kwenye karne ya 7 kulipelekea upatikanaji wa bidhaa mpya kama vile vitu vya chakula, mavazi, ngamia, bunduki na unga wa bunduki. Katika njiapanda hii, ukuaji wa biashara ukawa hauepukiki tena.
Ujio wa Waarabu katika Afrika ya Kaskazini hasa kwenye karne ya 7 kulipelekea upatikanaji wa bidhaa mpya kama vile vitu vya [[chakula]], [[mavazi]], ngamia, bunduki na [[unga wa bunduki]]. Katika njiapanda hii, ukuaji wa biashara ukawa hauepukiki tena.
;G) '''Uongozi mzuri wa falme'''
;G) '''Uongozi mzuri wa falme'''
Karibia falme zote hasa huko Afrika Magharibi ilikuwa na viongozi wazuri waliokuwa wanatoa hamasa ya ukuaji wa biashara. Falme kama ya Ghana na Mali zilitoa mpangilio mzuri wa biashara.
Karibia falme zote hasa huko Afrika Magharibi zilikuwa na viongozi wazuri waliokuwa wanatoa [[hamasa]] ya ukuaji wa biashara. Falme kama ya Ghana na Mali zilitoa mpangilio mzuri wa biashara.

==Sababu zilizopelekea kuanguka kwa biashara==
==Sababu zilizopelekea kuanguka kwa biashara==
Mwishoni mwa [[karne ya 14]], idadi ya misara ya biashara ikaanza kuanguka. Zifuatazo zilikuwa sababu kuu zilizopelekea kuanguka kwa biashara ya ng'ambo:
Mwishoni mwa [[karne ya 14]], idadi ya misafara ya biashara ikaanza kuanguka. Zifuatazo zilikuwa sababu kuu zilizopelekea kuanguka kwa biashara ya ng'ambo:
;A) '''Pepo kali za jangwani'''
;A) '''Pepo kali za jangwani'''
Wafanyabiashara wengi walitelekeza biashara zao kwa kufuatia upepo mkali uliokuwa unavuma jangwani. Pepo hizi zilifanya ugumu sana wa ukuaji na uendelezaji wa biashara.
Wafanyabiashara wengi walitelekeza biashara zao kwa kufuatia [[upepo]] mkali uliokuwa unavuma jangwani. Pepo hizi zilifanya ugumu sana wa ukuaji na uendelezaji wa biashara.
;B) '''Uvamizi wa Walmoravidi'''
;B) '''Uvamizi wa Walmoravidi'''
Hawa walikuwa Waarabu wanaotoka Mashariki ya Kati na wakataka kueneza Uislamu mjini Kaskazini na Magharibi mwa Afrika kwa mabavu. Hili nalo lilipelekea kudhoofisha biashara.
Hawa walikuwa Waarabu wa kutoka [[Mashariki ya Kati]], wakataka kueneza [[Uislamu]] mjini Kaskazini na Magharibi mwa Afrika kwa mabavu. Hili nalo lilipelekea kudhoofisha biashara.
;C) '''Vita vitakatifu'''
;C) '''Vita vitakatifu'''
Hivi vilikuwa vita baina ya Waislamu na hao wasiokuwa wanataka kufuata dini utamaduni wa Kiislamu hasa katika upande wa Afrika ya Magharibi. Matokeo yake, Vita vitakatifu hivi vimefanya ugumu wa uwepo wa amani na utulivu ndani ya misafara ya biashara na hivyo basi biashara ikaanguka.
Hivi vilikuwa vita baina ya Waislamu na hao wasiotaka kufuata [[dini]] na [[utamaduni]] wa Kiislamu, hasa upande wa Afrika ya Magharibi. Matokeo yake, [[Vita vitakatifu]] hivi vimefanya ugumu wa uwepo wa [[amani]] na [[utulivu]] ndani ya misafara ya biashara na hivyo basi biashara ikaanguka.
;D) '''Ujio wa Wazaungu'''
;D) '''Ujio wa Wazungu'''
Ujio wa Wazungu katika upande wa Kaskazini na Magharibi mwa Afrika kulipelekea muendelezo wa migogoro kwa vile Wazungu nao walitaka kueneza Ukristo na kushikiria biashara zote za misafara hii. Hili nalo lilichangia mazima katika kubomoa biashara.
Ujio wa [[Wazungu]] upande wa Kaskazini na Magharibi mwa Afrika kulipelekea muendelezo wa migogoro kwa vile Wazungu nao walitaka kueneza [[Ukristo]] na kushikilia biashara zote za misafara hii. Hili nalo lilichangia mazima katika kubomoa biashara.
;E) '''Kuanguka kwa falme'''
;E) '''Kuanguka kwa falme'''
Kuanguka kwa baadhi ya falme kama vile Ghana na Mali nako kulichangia kudidimia kwa biashara kutokana na ukweli wa kwamba falme hizi zilitoa mwongozo wa kibiashara kupitia viongozi wao ambao walikuwa wanawasimamia wafanyabiashara.
Kuanguka kwa baadhi ya falme, kama vile Ghana na Mali, nako kulichangia kudidimia kwa biashara kutokana na ukweli wa kwamba falme hizi zilitoa mwongozo wa kibiashara kupitia viongozi wao ambao walikuwa wanawasimamia wafanyabiashara.
;F) '''Kuibuka kwa [[Biashara ya utumwa ya ng'ambo ya Atlantiki]]'''
;F) '''Kuibuka kwa [[Biashara ya utumwa kupitia Atlantiki]]'''
Kuibuka kwa biashara ya pembetatu mwishoni mwa [[karne ya 15]] kulichangia kwa kuanguka mazima kwa biashara ya ng'ambo ya Sahara ambapo biashara ilihamia huko [[Amerika]] na [[Ulaya]].
Kuibuka kwa [[biashara ya pembetatu]] mwishoni mwa [[karne ya 15]] kulichangia kuanguka mazima kwa biashara ya ng'ambo ya Sahara ambapo biashara ilihamia huko [[Amerika]] na [[Ulaya]].

==Matokeo ya biashara ya ng'ambo ya Sahara==
==Matokeo ya biashara ya ng'ambo ya Sahara==
Biasha ya ng'ambo ya Sahara ilikuwa na matokeo (madhara) kadha wa kadha kwa Afrika Magharibi na Kaskazini kwa ujumla. Baadhi ya matokeo hayo ni pamoja na:
Biashara ya ng'ambo ya Sahara ilikuwa na matokeo (ma[[dhara]]) kadha wa kadha kwa Afrika Magharibi na Kaskazini kwa ujumla. Baadhi ya matokeo hayo ni haya:
===(i)Utambulisho wa tamaduni mpya===
===(i)Utambulisho wa tamaduni mpya===
Biashara ilileta tamaduni mpya kwa Afrika Magharibi na Kaskazini. Miongoni mwa tamaduni hizo ni pamoja na mtindo wa mavazi, vyakula, lugha na vingine vingi viliingia katika ukanda huu.
Biashara ilileta tamaduni mpya kwa Afrika Magharibi na Kaskazini. Miongoni mwa tamaduni hizo ni [[mtindo]] wa mavazi, vyakula, [[lugha]] na vingine vingi vilivyoingia katika ukanda huu.
===(ii)Ongezeko la watu===
===(ii)Ongezeko la watu===
Biashara pia ilipelekea kuongezeka kwa watu katika Afrika Magharibi na Kaskazini hasa kwa ujio wa Waarabu na watu wengine kutoka sehemu mbalimbali.
Biashara pia ilipelekea kuongezeka kwa watu katika Afrika Magharibi na Kaskazini hasa kwa ujio wa Waarabu na watu wengine kutoka sehemu mbalimbali.
===(iii)Ukuaji wa miji na vijiji===
===(iii)Ukuaji wa miji na vijiji===
Biashara ya Ng'ambo ilichangia kwa kiasi kikubwa katika maendeleo ya miji na vijiji katika Afrika Magharibi na Kaskazini - kama vile [[Timbuktu]], [[Mandika]], [[Kumbi Saleh]], [[Taghaza]] na [[Tripoli]] na mingine mingi.
Biashara ya Ng'ambo ilichangia kwa kiasi kikubwa katika [[maendeleo]] ya miji na [[kijiji|vijiji]] katika Afrika Magharibi na Kaskazini - kama vile [[Timbuktu]], [[Mandika]], [[Kumbi Saleh]], [[Taghaza]], [[Tripoli]] na mingine mingi.
===(iv)Uenezi wa dini Kiislamu===
===(iv)Uenezi wa dini ya Kiislamu===
Biashara pia ilipelekea kuenea kwa dini ya [[Uislamu|Kiislamu]] kwa Afrika Magharibi na Kaskazini kwa ujumla - ambapo baadhi ya Waafrika walitelekeza dini zao za jadi na kujiunga na Uislamu.
Biashara pia ilipelekea kuenea kwa dini ya [[Uislamu|Kiislamu]] kwa Afrika Magharibi na Kaskazini kwa ujumla - ambapo baadhi ya Waafrika walitelekeza [[dini asilia za Kiafrika|dini zao za jadi]] na kujiunga na Uislamu.
===(v)Ndoa mseto===
===(v)Ndoa mseto===
Ndoa za mseto zilitokea baina ya Waafrika kutoka Magharibi na hao kutoka Kaskazini kwa kufuatia biashara hii. Vilevile ndoa mseto zilitokea baina ya Waarabu na Waafrika.
[[Ndoa za mseto]] zilitokea baina ya Waafrika kutoka Magharibi na hao kutoka Kaskazini kwa kufuatia biashara hii. Vilevile ndoa za mseto zilitokea baina ya Waarabu na Waafrika.
===(vi)Ukuaji wa falme/madola===
===(vi)Ukuaji wa falme/madola===
Biashara pia ilipelekea kukua kwa falme nyingi huko Kaskazini na Magharibi mwa Afrika. Baadhi ya madola na falme hizo ni pamoja na Ghana na Mali.
Biashara pia ilipelekea kukua kwa falme nyingi huko Kaskazini na Magharibi mwa Afrika. Baadhi ya madola na falme hizo ni Ghana na Mali.
===(vii)Kuibuka kwa viongozi na wafanyabiashara wakubwa===
===(vii)Kuibuka kwa viongozi na wafanyabiashara wakubwa===
Biashara ya ng'ambo ilipelekea kuibuka kwa viongozi wenye nguvu (athira/ushawishi) mkubwa hasa katika upande wa Magharibi. Viongozi hao ni pamoja na [[Sundiata Keita]], [[Mansa Mussa]], [[Askia Muhammad]] na [[Sunni Ali]].
Biashara ya ng'ambo ilipelekea kuibuka kwa viongozi wenye nguvu ([[athira]]/[[ushawishi]]) mkubwa hasa upande wa Magharibi. Viongozi hao ni pamoja na [[Sundiata Keita]], [[Mansa Mussa]], [[Askia Muhammad]] na [[Sunni Ali]].

==Tazama pia==
==Tazama pia==
*[[Biashara ya masafa marefu ya Afrika Mashariki]]
*[[Biashara ya masafa marefu ya Afrika Mashariki]]
Mstari 79: Mstari 90:
*[[Historia ya Afrika]]
*[[Historia ya Afrika]]
*[[Historia ya Ghana]]
*[[Historia ya Ghana]]
*[[Historia ya Senegal]]
*[[Historia ya Mali]]


==Jisomee==
==Jisomee==
Mstari 95: Mstari 106:


[[Jamii:Historia ya Afrika]]
[[Jamii:Historia ya Afrika]]
[[Jamii:Biashara]]
[[Jamii:Utumwa]]

Pitio la 14:30, 2 Agosti 2015

Oasisi ya Bilma mjini kaskazinimashariki mwa Niger, kukiwa na mharara wa Kaouar kwa nyuma

Biashara ya ng'ambo ya Sahara (vilevile Biashara ya Masafa Marefu ya Afrika ya Magharibi) ilikuwa biashara iliyohusisha Afrika ya Magharibi na Afrika ya Kaskazini kupitia jangwa la Sahara.

Biashara hiyo ni mfano mzuri wa biashara za kanda au masafa marefu ambayo yaliongozwa katika upande wa Afrika Magharibi.

Biashara hiyo ilianza mnamo karne ya 4 na iliendelea zaidi hadi katika karne ya 17 ambapo ilianguka mazima.

Biashara ilikuwa na matokeo kadha wa kadha katika historia ya Afrika Magharibi na ya Afrika kwa ujumla.

Historia

Washiriki

Washirika wakubwa wa biashara hii walikuwa watu kutoka Mataifa ya Kimagharibi ya Sudani, Ghana, Mali na Songhai na baadhi ya watu kutoka mjini Kaskazini mwa Afrika.

Kutoka Afrika Magharibi

Ilihusisha kikundi cha Wasoninke, Wamandika, Wayoruba, Wafulani, Wahausa na wengineo wengi.

Kutoka Afrika Kaskazini

Ilihusisha kikundi cha Waarabu, Waberberi, Watuareki na wengine wengi.

Bidhaa au vitu vilivyokuwa vinauzwa

Bidhaa zilizokuwa zinauzwa ni mchanganyiko, lakini vilevile mauzo yaliendana na kanda. Mifano:

Kutoka Afrika Magharibi

Kutoka ndanindani kabisa ya misitu ya Afrika Magharibi, bidhaa zilikuwa dhahabu, fedha, ngozi za wanyama, pembe za ndovu, nta ya nyuki, asali and vitu vingine vya thamani vilivyoweza kubebwa.

Kutoka Afrika Kaskazini

Kutoka Kaskazini, Waberberi na Waarabu walileta bidhaa ndogondogo kwa mfano shanga, miwani, silaha na vingine vingi. Kwa upande wa jangwa la Sahara chumvi ilikuwa inapatikana kutoka Taghaza, Fez na Bilima. Aina kuu za usafiri wakati wa biashara hii ilikuwa punda, farasi na wakati mwingine walitembea kwa miguu. Lakini baadaye katika karne ya 7, ngamia waliletwa na Waarabu ambao waliwasili wakitokea Mashariki ya Kati na kuanza kutumika kama chombo kikuu cha usafiri kupitia Sahara.

Muundo wa biashara

Biashara ilipangwa kwa mtindo wa misafara kama msururu ambayo ilianza kutoka kila upande wa Magharibi na Kaskazini mwa Afrika kupitia jangwa la Sahara. Misafara hiyo ilikuwa kama ifuatavyo:

(a) Msafara wa Magharibi

Msafara ulianza kutoka Sijilmasa na Fez huko nchini Morocco. Halafu ukapitia Taghaza, Taoden, Watala, Audaghost, Kumbi Saleh hadi Timbuktu.

(b) Msafara wa Kati

Msafara ulianza kutoka Tunis wakapitia Ghat, Kano kisha ukaenda zake na kupitia jangwani hadi Gao na mwisho kabisa Hausa.

(c) Msafara wa Mashariki

Msafara huu ulianzia mjini Tripoli ukaenda zake hadi Marzul na mwisho kabisa ukamalizikia mjini Bilima.

Sababu zilizopelekea kukua kwa biashara

Msafara wa ngamia wa siku hizi karibu na Milima ya Ahaggar katikati ya jangwa la Sahara, 2006.

Ukuaji na uendeleaji wa Biashara ya Ng'ambo ya Sahara iliathiriwa na mambo kadha wa kadha. Miongoni mwa sababu hizo ni:

A) Siasa Imara

Katika nchi za Magharibi na Kaskazii hali ilikuwa shwari kabisa, hakukuwa na vita wala nini. Hili lilitoa chumba cha ukuaji wa biashara ya ng'ambo.

B) Eneo la Kijiografia

Mahali penyewe panawezesha maendeleo ya kibiashara. Hili lilitokana na ukweli ni kwamba Magharibi na Kaskazini mwa Afrika zimepakana mno kupitia jangwa la Sahara.

C) Upatikanaji wa bidhaa

Upatikanaji wa bidhaa huko Magharibi na Kaskazini mwa Afrika kulipelekea kukua kwa biashara ya ng'ambo.

D) Utambulishaji wa ngamia kama zana ya kusarishia

Ngamia alitambulishwa na Waarabu kama zana kuu ya kusafirishia kupitia jangwa la Sahara katika karne ya 7. Hili lilirahisha shughuli za usafirishaji kupitia jangwani hivyo basi kupelekea ongezeko la ukuaji wa biashara hii.

E) Uwepo wa chemchemi jangwani

Haya ni maeneo ya jangwa yenye vyanzo vya maji. Uwepo wa maeneo haya yenye maji umepelekea upatikanaji wa maji hayo kwa ajili ya ngamia na wafanyabiashara, hivyo kuzidi kuchochea maendeleo ya ukuaji wa kibiashara.

F) Ujio wa Waarabu

Ujio wa Waarabu katika Afrika ya Kaskazini hasa kwenye karne ya 7 kulipelekea upatikanaji wa bidhaa mpya kama vile vitu vya chakula, mavazi, ngamia, bunduki na unga wa bunduki. Katika njiapanda hii, ukuaji wa biashara ukawa hauepukiki tena.

G) Uongozi mzuri wa falme

Karibia falme zote hasa huko Afrika Magharibi zilikuwa na viongozi wazuri waliokuwa wanatoa hamasa ya ukuaji wa biashara. Falme kama ya Ghana na Mali zilitoa mpangilio mzuri wa biashara.

Sababu zilizopelekea kuanguka kwa biashara

Mwishoni mwa karne ya 14, idadi ya misafara ya biashara ikaanza kuanguka. Zifuatazo zilikuwa sababu kuu zilizopelekea kuanguka kwa biashara ya ng'ambo:

A) Pepo kali za jangwani

Wafanyabiashara wengi walitelekeza biashara zao kwa kufuatia upepo mkali uliokuwa unavuma jangwani. Pepo hizi zilifanya ugumu sana wa ukuaji na uendelezaji wa biashara.

B) Uvamizi wa Walmoravidi

Hawa walikuwa Waarabu wa kutoka Mashariki ya Kati, wakataka kueneza Uislamu mjini Kaskazini na Magharibi mwa Afrika kwa mabavu. Hili nalo lilipelekea kudhoofisha biashara.

C) Vita vitakatifu

Hivi vilikuwa vita baina ya Waislamu na hao wasiotaka kufuata dini na utamaduni wa Kiislamu, hasa upande wa Afrika ya Magharibi. Matokeo yake, Vita vitakatifu hivi vimefanya ugumu wa uwepo wa amani na utulivu ndani ya misafara ya biashara na hivyo basi biashara ikaanguka.

D) Ujio wa Wazungu

Ujio wa Wazungu upande wa Kaskazini na Magharibi mwa Afrika kulipelekea muendelezo wa migogoro kwa vile Wazungu nao walitaka kueneza Ukristo na kushikilia biashara zote za misafara hii. Hili nalo lilichangia mazima katika kubomoa biashara.

E) Kuanguka kwa falme

Kuanguka kwa baadhi ya falme, kama vile Ghana na Mali, nako kulichangia kudidimia kwa biashara kutokana na ukweli wa kwamba falme hizi zilitoa mwongozo wa kibiashara kupitia viongozi wao ambao walikuwa wanawasimamia wafanyabiashara.

F) Kuibuka kwa Biashara ya utumwa kupitia Atlantiki

Kuibuka kwa biashara ya pembetatu mwishoni mwa karne ya 15 kulichangia kuanguka mazima kwa biashara ya ng'ambo ya Sahara ambapo biashara ilihamia huko Amerika na Ulaya.

Matokeo ya biashara ya ng'ambo ya Sahara

Biashara ya ng'ambo ya Sahara ilikuwa na matokeo (madhara) kadha wa kadha kwa Afrika Magharibi na Kaskazini kwa ujumla. Baadhi ya matokeo hayo ni haya:

(i)Utambulisho wa tamaduni mpya

Biashara ilileta tamaduni mpya kwa Afrika Magharibi na Kaskazini. Miongoni mwa tamaduni hizo ni mtindo wa mavazi, vyakula, lugha na vingine vingi vilivyoingia katika ukanda huu.

(ii)Ongezeko la watu

Biashara pia ilipelekea kuongezeka kwa watu katika Afrika Magharibi na Kaskazini hasa kwa ujio wa Waarabu na watu wengine kutoka sehemu mbalimbali.

(iii)Ukuaji wa miji na vijiji

Biashara ya Ng'ambo ilichangia kwa kiasi kikubwa katika maendeleo ya miji na vijiji katika Afrika Magharibi na Kaskazini - kama vile Timbuktu, Mandika, Kumbi Saleh, Taghaza, Tripoli na mingine mingi.

(iv)Uenezi wa dini ya Kiislamu

Biashara pia ilipelekea kuenea kwa dini ya Kiislamu kwa Afrika Magharibi na Kaskazini kwa ujumla - ambapo baadhi ya Waafrika walitelekeza dini zao za jadi na kujiunga na Uislamu.

(v)Ndoa mseto

Ndoa za mseto zilitokea baina ya Waafrika kutoka Magharibi na hao kutoka Kaskazini kwa kufuatia biashara hii. Vilevile ndoa za mseto zilitokea baina ya Waarabu na Waafrika.

(vi)Ukuaji wa falme/madola

Biashara pia ilipelekea kukua kwa falme nyingi huko Kaskazini na Magharibi mwa Afrika. Baadhi ya madola na falme hizo ni Ghana na Mali.

(vii)Kuibuka kwa viongozi na wafanyabiashara wakubwa

Biashara ya ng'ambo ilipelekea kuibuka kwa viongozi wenye nguvu (athira/ushawishi) mkubwa hasa upande wa Magharibi. Viongozi hao ni pamoja na Sundiata Keita, Mansa Mussa, Askia Muhammad na Sunni Ali.

Tazama pia

Jisomee