Jumuiya ya Nchi Huru

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Bendera ya Jumuiya ya Nchi Huru
Nchi wanachama wa Jumuiya ya Nchi Huru;
dhambarau: wanachama kamili;
dhambarau nyeupe: wanachama washirikishwa

Jumuiya ya Nchi Huru (Kirusi Содружество Независимых Государств (СНГ) sodrushestvo nezavisimikh gosudarstv (SNG); Kiing. Commonwealth of Independent States (CIS)) ni jina la umoja wa nchi zilizokuwa sehemu za Umoja wa Kisovyeti hadi 1991.

Jumuiya hii iliundwa tar. 8 desemba 1991 na viongozi wa Urusi, Belarusi na Ukraine. Makao makuu yapo Minsk kwenye mji mkuu wa Belarusi na mkutano wa wabunge hukutana Sankt Peterburg.

Wanachama

+Nchi mwanachama wa kushirikishwa

+ Nchi zilizokuwa jamhuri za Umoja wa Kisovyeti zisizoshiriki katika jumuiya

Shabaha na hali ya jumuiya

Jumuiya ilianzishwa kama njia ya kuondoa Umoja wa Kisovyeti bila kuacha ushirikiano. Tangu kuundwa nchi wanachama zilitia sahihi kwenye mikataba na mapatano mengi lakini hali halisi umuhimu wa umoja huu umerudi nyuma. Maraisi hawakukutana pamoja tangu miaka kadhaa.

Ukraine na Georgia zinaelekea kujiunga na Ulaya na kambi la magharibi pamoja na NATO na mwelekeo huu umeshasababisha ugomvi na Urusi. Moldavia vilevile inaimarisha uhusiano wake na Romania hasa ambayo ni mwanachama wa Umoja wa Ulaya na NATO kwa sababu Wamoldavia wengi huongea Kiromania.


Viungo vya Nje