Nenda kwa yaliyomo

Minsk

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Kanisa la Roho Mtakatifu mjini Minsk
Uwanja wa Ushindi katikati ya mji wa Minsk

Minsk au Miensk (Мінск (Kibelarus) ni mji mkuu na mji mkubwa nchini Belarus. Idadi ya wakazi ni watu milioni 1.8. Mji ulikua kando la mto Svislach.

Jina la mji wa Minsk lilitajwa mara ya kwanza mwaka 1067. Mwaka 1326 ulikuwa sehemu ya dola la Lithuania ukapata cheo cha mji mwaka 1499. Tangu 1793 Minsk ilikuwa sehemu ya Dola la Urusi.

Baada ya mapinduzi ya kikomunisti Minsk ilikuwa mji mkuu wa Jamhuri ya Kisoshalisti ya Kisovyeti ya Belorus ndani ya Umoja wa Kisovyeti.

Makala hii kuhusu maeneo ya Ulaya bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Minsk kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.