Vladimir Putin

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Vladimir Putin na bendera ya Urusi.

Vladimir Vladimirovich Putin (kwa Kirusi Владимир Владимирович Путин; amezaliwa 7 Oktoba 1952) ni mwanasiasa nchini Urusi. Mara tatu alichaguliwa kuwa Rais wa Shirikisho la Urusi, mara ya mwisho tarehe 7 Mei 2012; awamu za kwanza zilikuwa kutoka 2000 hadi 2008. Kuanzia Agosti 1999 hadi Mei 2000, tena kuanzia 2008 hadi 2012 alikuwa waziri mkuu wa Urusi.

Alikaimu kiti cha Urais tarehe 31 Desemba 1999, pale rais Boris Yeltsin alijiuzulu kwa ghafla. Kisha Putin akashinda uchaguzi wa rais mnamo mwaka wa 2000. Mnamo mwaka wa 2004, alichaguliwa upya na kushinda, hivyo aliendelea na kipindi chake cha pili hadi tarehe 7 Mei 2008.

Administradors.png Makala hii kuhusu mwanasiasa fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Vladimir Putin kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.