Historia ya Iraq
Historia ya Iraq inahusu eneo ambalo leo linaunda Jamhuri ya Iraq.
Mesopotamia ina historia ndefuː ilikuwa kitovu cha ustaarabu wa binadamu, mahali pa miji ya kwanza duniani katika Sumeri na Babeli.
Baada ya kusambaratika kwa milki ya Waturuki Waosmani walioitawala muda mrefu, Iraq ilikubaliwa kuwa mwanachama wa Shirikisho la Mataifa mwaka 1932 ingawa hali halisi ilikuwa nchi lindwa chini ya athira ya Uingereza hadi mwaka 1958.
Miaka ya hivi karibuni imejulikana hasa kutokana na vita mbalimbaliː kwanza vita dhidi ya Uajemi chini ya serikali ya Saddam Hussein tangu 1981, baadaye vita dhidi ya Kuwait na Marekani.
Vita vya pili vya Ghuba ya 2003 vilivyoleta uvamizi wa Marekani vilizidi kuleta vifo na uharibifu.
Hatimaye vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyoingiliwa na DAESH iliyoteka sehemu kubwa ya nchi, hasa kaskazini na magharibi, hadi iliposhindwa mwaka 2017.
Makala hii kuhusu mambo ya kihistoria bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Historia ya Iraq kama enzi zake au matokeo yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |