Ukristo barani Amerika

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru


Ukristo barani Amerika uliingia mara Wazungu walipofikia huko. Kabla ya hapo wakazi walifuata dini za jadi, zikiheshimu roho na uasilia, lakini pengine zikidai pia binadamu atolewe kama kafara.

Kati ya Wazungu walioongozana na Kristofa Columbus kulikuwa na mapadri waliokuwa tayari kufanya umisionari walifika kaskazini kabisa mwa bara.

Kwa kiasi kikubwa uinjilishaji uliendana na ukoloni wa karne XVI na XVII: katika sehemu mbalimbali wahamiaji wengi kutoka Ulaya walizidi idadi ya wenyeji, lakini pia hawa wa mwisho waliingia Ukristo kwa wingi.

Matokeo ni kwamba leo Amerika ndilo bara lenye asilimia kubwa zaidi za Wakristo, wakiwemo hasa Wakatoliki na Waprotestanti, lakini pia Waorthodoksi, Waorthodoksi wa Mashariki na madhehebu mengine ambayo yalitokea Marekani hasa katika karne ya 19.

Makala hii kuhusu dini ya Ukristo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Ukristo barani Amerika kama historia yake, matokeo au athari zake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.