Kanisa la Moravian Tanzania
Kanisa la Moravian Tanzania (kifupisho: KMT) ni muungano wa majimbo ya Kanisa la Moravian nchini Tanzania. Idadi ya Wakristo wake imekadiriwa kuwa 738,000. Makao makuu yako Mbeya mjini.
Kwa pamoja KMT inaendesha Chuo Kikuu Teofilo Kisanji.
Kazi nyingine ya pamoja ni kutolewa kwa "Kiongozi Kalenda" ambayo ni chaguo la maneno ya Biblia kwa kila siku.
Majimbo ya KMT
[hariri | hariri chanzo]Kuna majimbo matano ya KMT ambayo ni
- Kanisa la Moravian Tanzania Jimbo la Kusini (Moravian Church in Southern Tanzania) - makao makuu ni Rungwe
- Kanisa la Moravian Tanzania Jimbo la Magharibi (Moravian Church in Western Tanzania) - makao makuu ni Tabora
- Kanisa la Moravian Tanzania Jimbo la Kusini Magharibi (Moravian Church in South-Western Tanzania) - makao makuu ni Mbeya Mjini
- Kanisa la Moravian Tanzania Jimbo la Rukwa (Moravian Church in Tanzania Rukwa Province) - makao makuu ni Sumbawanga
- Kanisa la Moravian Tanzania Jimbo la Ziwa Tanganyika (Moravian Church in Tanzania Lake Tanganyika Province)- makao makuu ni Kigoma
Kila jimbo ni kanisa kamili la kujitegemea.
Pamoja na hayo kuna majimbo mawili ya misheni ambayo hayajafikia hali ya kujitegemea kikamilifu, hivyo bado yanashirikiana kila moja na jimbo mzazi. Hayo ni
- Jimbo la Misheni Mashariki ya Tanzania na Zanzibar (mzazi: Jimbo la Kusini - Rungwe)
- Jimbo la Misheni Kaskazini (mzazi: Jimbo la Kusini Magharibi - Mbeya).
- Jimbo la Misheni Kusini Magharibi Iringa (mzazi: Jimbo la Kusini Magharibi - Mbeya)
Historia
[hariri | hariri chanzo]Kazi ya Wamoravian ilianza Tanzania mnamo mwaka 1891 wamisionari wa kwanza kutoka Ujerumani walipofika Rungwe katika eneo la Wanyakyusa. Kutoka Unyakyusa kazi ilipanuka kwa kuunda vituo huko Utengule (Mbeya)]] (kwa Wasafwa) na Mbozi (kwa Wanyiha).
Kazi katika magharibi ya nchi ilianza mwaka 1897 Wamoravian walipokabidhiwa kituo cha Urambo kilichowahi kuanzishwa na shirika la misioni la London (LMS).
Ndiyo chanzo cha majimbo ya Kusini (Rungwe) na Magharibi (Tabora).
Jimbo la Kusini Magharibi lilitengwa na lile la Kusini mwaka 1976.
Jimbo la Rukwa lilijitegemea na lile la Tabora mnamo 1986.
Jimbo la Ziwa Tanganyika lilianzishwa rasmi mwaka 2013.
Hasa katika mkoa wa Mbeya kanisa la Moravian ni kubwa kati ya madhehebu ya Kiprotestanti.
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- Tovuti ya KMT pamoja na majimbo ya Morabian Tanzania Ilihifadhiwa 26 Februari 2011 kwenye Wayback Machine.
- Ukurasa wa KMT Ilihifadhiwa 16 Mei 2011 kwenye Wayback Machine.
- Orodha ya watendaji na vitengo vya KMT Ilihifadhiwa 1 Januari 2011 kwenye Wayback Machine.
Makala hii kuhusu dini ya Ukristo bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Kanisa la Moravian Tanzania kama historia yake, matokeo au athari zake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |