Wanyakyusa
Wanyakyusa (pia huitwa Wangonde au Wasochile) ni jina kwa ajili ya watu wanaoishi kwenye wilaya ya Rungwe katika sehemu za kusini za Mkoa wa Mbeya (Tanzania) upande wa kaskazini ya Ziwa Nyasa. Lugha yao ni Kinyakyusa. Mara nyingi Wagonde upande wa kusini ya mto Songwe nchini Malawi huhesabiwa pamoja nao katika kundi lilelile.
Kihistoria watu wanaoitwa leo Wanyakyusa waliitwa Wakonde na Wanyakyusa walikuwa kabila kubwa kati yao. Wakati wa karne ya 20 "Wanyakyusa" imekuwa jina la kundi kwa jumla. Hadi leo kanisa la kilutheri la KKKT linatumia jina "dayosisi ya Konde" kwa eneo lake katika mkoa wa Mbeya.
Wakati Wajerumani walipofika sehemu za kaskazini ya Ziwa Nyasa mwisho wa karne ya 19 hawakuona tofauti ya kimsingi kati ya watu wa Malawi kaskazini na wale wa sehemu za Rungwe wakawaita wote "Wakonde" kutokana na jina lililokuwa kawaida ziwani.
Leo hii ni watu zaidi ya milioni wanaojumlishwa kwa jina hili, takriban 700,000 wanaokaa upande wa Tanzania na 300,000 wakikaa Malawi.
[hariri] Viungo vya Nje
- The Nyakyusa Homepage
- "Wakonde" katika Kamusi ya Koloni za Kijerumani (1920)
- Marcia Right, Nyakyusa Cults and Politics in the later Nineteenth Century; in: Ranger - Kimambo, The Historical Study of African Religion, Berkeley & Los Angeles 1972 (google book review)
| Makala hii kuhusu utamaduni wa Tanzania bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Wanyakyusa kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |