Nenda kwa yaliyomo

Jomo Kenyatta

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jomo Kenyatta


Muda wa Utawala
12 Desemba 1964 – 22 Agosti 1978
mtangulizi (rais wa kwanza)
aliyemfuata Daniel arap Moi

Waziri Mkuu wa Kenya
Muda wa Utawala
1 Juni 1963 – 12 Desemba 1964
mtangulizi (gavana) Malcolm MacDonald
aliyemfuata Raila Odinga

tarehe ya kuzaliwa 1894[1]
Ichaweri, Gatundu, British East Africa
tarehe ya kufa 22 Agosti 1978 (umri 83)
Mombasa, Kenya
chama KANU
ndoa Grace Wahu (m. 1919),
Edna Clarke (1942-1946),
Grace Wanjiku,
Mama Ngina (1951-1978)

Jomo Kenyatta (1893-1978) alikuwa rais wa kwanza wa Kenya.

Jina lake halisi lilikuwa Johnstone Kamau wa Ngengi. Alipewa jina la utani ambalo ni Mkuki wa Moto (Burning Spear). Jina la Kenyatta lilitokana na mkanda aliopenda kuuvaa ambao ulitengenezwa kwa shanga. Wagĩkũyũ wanauita kenyaata.

Maisha

Alisoma katika shule ya kanisa la wamisionari wa Kiskoti.

Baada ya kuhitimu aliajiriwa kama karani na msoma mita wa manispaa ya Nairobi, alioa mke wake wa kwanza ambaye ni Grace Wahu.

Kabila lake lilikuwa ni Mgĩkũyũ. Azma yake ya kutaka kuikomboa ardhi ya Wagĩkũyũ ilimfanya aweze kuwaunganisha, naye akawa katibu wao mwaka 1928.

Mwaka 1930 alizuru Marekani na Uingereza ambako aliishi miaka kumi na mitano na hata kuoa mwalimu wa Kiingereza ambaye aliitwa Edna Kenyatta.

Alirudi Kenya mwaka 1946 na alichaguliwa kuwa rais wa chama cha siasa cha Kenya African Union (KANU). Alihamasisha kukomeshwa ubaguzi wa rangi; kuwa na mwamko kisiasa pamoja na mambo mengine yanayompa Mwafrika heshima na utu.

Aliandika kitabu kiitwacho Facing Mount Kenya kilichohusu ukombozi na historia ya Wagĩkũyũ. Alikuwa pia mwanzilishi na mhariri wa gazeti la kwanza kwa lugha ya Gĩkũyũ ambalo liliitwa Mũigũithania.

Kutokana na kuhusishwa na harakati za vita vya msituni vya kundi la Mau Mau alihukumiwa miaka saba jela mwaka 1952. Huwezi kuzungumza historia ya Kenyatta bila ya kuitaja Maumau.

Baadaye alioa mke wa tatu aliyeitwa Mama Ngina Kenyatta ambaye alikuja kuwa mke wa rais wa kwanza na ambaye ndiye mama yake Uhuru Kenyatta, rais wa sasa.

Licha ya Waingereza kuwa na matumaini ya kuwapa wapinzani Waafrika mamlaka "ya wastani" zaidi, ilikuwa Kenya African National Union (KANU) ya Jomo Kenyatta, mfungwa wa zamani, ambayo iliunda serikali muda mfupi kabla ya Kenya kupata uhuru tarehe 12 Desemba 1963.

Tarehe 1 Juni 1963 Kenya ilipata madaraka na Jomo Kenyatta alitawazwa kuwa Waziri Mkuu wa kwanza wa Kenya.

Mwaka mmoja baadaye, Kenyatta akawa rais wa kwanza wa Kenya juu ya uanzishwaji wa jamhuri.

Chama kidogo cha Kenya African Democratic Union (KADU), kilichowakilisha muungano wa makabila madogo ambayo yaliogopa utawala wa makabila makubwa, kilijitoa na kujivunja mwaka wa 1964 na wanachama wake wakajiunga na KANU.

Chama kidogo cha upinzani, Kenya People's Union (KPU), kilianzishwa mwaka 1966, kiongozi wake akiwa Jaramogi Oginga Odinga aliyewahi kuwa makamu wa rais Kenyatta. KPU ilipigwa marufuku, na kiongozi kuwekwa kizuizini baada ya chachari za kisiasa zilizohusishwa na ziara za Kenyatta katika Mkoa wa Nyanza. Hakuna vyama vingine vya upinzani vilivyoanzishwa baada ya 1969, kupelekea Kenya kuwa mfumo wa chama kimoja chini ya KANU.

Kenyatta alifariki mjini Mombasa tarehe 18 Agosti 1978 na kuzikwa jijini Nairobi kwenye jengo la bunge.

Marejeo

  1. "Dukier World History, 4th edition, 2004"