Historia ya Kenya

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta

Historia ya Kenya, kama nchi inayokaliwa na binadamu, inaenea mamilioni ya miaka, ingawa historia ya Kenya kama nchi huru ni fupi.

Historia ya awali ya Kenya[hariri | hariri chanzo]

Uvumbuzi wa majuzi karibu na Ziwa Turkana unaonyesha kwamba kiumbe kama Australopithecus anamensis aliishi katika eneo ambalo sasa ni Kenya kuanzia miaka milioni 4.1 iliyopita. Lakini mabaki yaliopatikana katika mabonde ya Tugen, yaliyokuwa na takriban miaka milioni 6, yalipelekea kutajwa kwa aina mpya ya spishi, Orrorin tugenensis.

Ustaarabu wa mapema Kenya[hariri | hariri chanzo]

Mahali pa Msikiti Mkuu wa Gedi, karne ya 13.

Wafanyabiashara Waarabu walianza kwenda pwani ya Kenya mara kwa mara karne ya 1 BK . Kenya ilikuwa karibu na Peninsula ya Arabia na hii ilialika ukoloni. Makazi ya Waarabu na Waajemi yaliongezeka kandokando ya pwani kufikia karne ya 8.

Kiswahili, lugha ya Afrika yenye maneno mengi yaliyokopwa kutoka Kiarabu, iliendelea kuwa kama lingua franca kwa sababu za kibiashara kati ya watu tofauti.

Utamalaki wa Waarabu katika eneo la pwani ulipitwa karne ya 16 na Wareno ambao utawala wao pia ulipisha Omani mwaka wa 1698.

Uingereza ulianzisha mvuto wake karne ya 19. Njia mojawapo ya kuanzisha mvuto huu ulikuwa kupitia wamisionari. Misheni ya kwanza ya Ukristo ilianzishwa tarehe 25 Agosti mwaka wa 1846, na Daktari Ludwig Krapf, Mjerumani na mtawa wa Church Missionary Society ya Uingereza, ambaye alijifahamisha kati ya Wamijikenda huko pwani. Baadaye alitafsiri Biblia kutoka Kiingereza hadi Kiswahili.

Historia ya ukoloni[hariri | hariri chanzo]

Historia ya ukoloni ya Kenya ilianza wakati milki ya Ujerumani ya nchi lindwa (protectorate) ilipoanzishwa. Nchi lindwa hii ilikuwa mali ya Sultani wa Pwani na Zanzibar na wakati huo ulikuwa mnamo 1885.

Hii ilifuatiwa na kuwasili kwa British East Africa Company (BEAC) ya Bwana William Mackinnon mwaka wa 1888, baada ya kampuni hii kupokea mkataba wa kifalme na haki za kuungama kwa pwani ya Kenya kutoka Sultani wa Zanzibar kwa kipindi cha miaka 50.

Uhasimu wa umilki ulinza kuonekana wakati Ujerumani ulipatiana sehemu yake ya pwani kwa milki ya Uingereza mwaka wa 1890, ndiposa uweze kuidhibiti pwani ya Tanganyika.

Kuhozi kwa ukoloni huu mara kwa mara ulikumbana na upinzani mbalimbali: Waiyaki Wa Henya, chifu Mkikuyu aliyetawala Dagoretti ambaye alikuwa amesaini mkataba na Frederick Lugard wa BEAC, baada ya kuteswa na kubughudhiwa, aliliteketeza gereza la Lugard mnamo 1890. Waiyaki alitekwa nyara miaka miwili baadaye na Waingereza na kuuawa.

Kufuatia matatizo ya kifedha ya British East African Company, serikali ya Uingereza ilianzisha utawala wa moja kwa moja kupitia nchi lindwa ya Afrika ya mashariki (East African Protectorate) mnamo tarehe 1 Julai 1895.

Hii ilifuatwa na ufunguzi wa nyanda kwa Wazungu walowezi mwaka wa 1902 . Ujenzi wa reli ulianza mwaka wa 1895 kutoka Mombasa hadi Kisumu katika ziwa Viktoria na ulimalizika mwaka wa 1901. Ujenzi huu uliwezesha wakoloni hao kuingia ndani kabisa mwa Kenya. Hii ilikuwa sehemu ya kwanza ya reli ya Uganda.

Katika ujenzi wa reli, Waingereza walikumbana na upinzani mgumu, hasa kutoka kwa Koitalel Arap Samoei, kiongozi wa Kinandi na mwaguzi aliyetabiri ya kwamba nyoka mweusi atapita katikati ya eneo la Nandi akitema mate ya moto. Nyoka alikuwa anaashiria reli. Kwa miaka kumi Samoei alipigana dhidi ya wajenzi wa reli na gari la moshi. Baadaye, Samoei aliuawa na Waingereza kwani walikuwa na dhamira ya kuendelea na kumaliza reli hii.

Walowezi waliruhusiwa kuingia bungeni na serikali mwaka wa 1907 kupitia Legislative Council, shirika la Ulaya ambalo baadhi ya walowezi waliasisiwa na wengine walichaguliwa. Lakini tangu mamlaka zaidi zilibakia katika mikono ya Gavana, walowezi walitaka Kenya ibadilishwe kuwa koloni la kiarauni au taji (Crown Colony), ambayo ilimaanisha mamlaka zaidi kwa walowezi.

Walowezi hao walihitimu lengo lao mwaka wa 1920 kwa kulifanya Baraza liwakilishwe na walowezi zaidi. Waafrika walitengwa kutoshiriki katika siasa ya moja kwa moja hadi mwaka wa 1944, ambapo mmojawao aliingizwa kwenye Baraza.

Wakikuyu waliamua kuanzisha chama chao cha kwanza cha kupinga harakati za kisiasa ambacho kiliitwa Young Kikuyu Association. Kiongozi wake alikuwa Harry Thuku. Sababu nyingine ya kuanzishwa kwa chama hiki ni kwamba Waafrika hawakuwa na mwakilishi katika siasa. Chama hicho kilianzishwa mwaka wa 1921. Baadaye jina la chama lilibadilishwa likawa Kenya African Union (KAU), shirika la kitaifa lilodai kuingia katika nchi iliyomilikwa na walowezi. Mwaka 1947, urais wa chama hiki ulitolewa kwa Jomo Kenyatta.

Kuanzia Oktoba 1952 mpaka Desemba 1959, Kenya ilikuwa katika hali ya hatari kufuatia uasi wa Mau Mau dhidi ya utawala wa Uingereza. Ushiriki wa Afrika katika mchakato wa kisiasa uliendelea kwa kasi katika sehemu ya mwisho ya muda huo kwani Waingereza walitaka kutenga wahalifu na wafuasi wao. Uchaguzi wa kwanza wa moja kwa moja wa Waafrika katika bunge ulifanywa mwaka wa 1957.

Kenya Huru[hariri | hariri chanzo]

Licha ya Waingereza kuwa na matumaini ya kuwapa wapinzani Waafrika mamlaka "ya wastani" zaidi , ilikuwa Kenya African National Union (KANU) ya Jomo Kenyatta, mwanachama wa kabila la Kikuyu na mfungwa wa zamani, ambayo iliunda serikali muda mfupi kabla ya Kenya kupata uhuru tarehe 12 Desemba 1963.

Mwaka mmoja baadaye, Kenyatta akawa rais wa kwanza wa Kenya juu ya uanzishwaji wa jamhuri.


Chama kidogo cha Kenya African Democratic Union (KADU), kilichowakilisha muungano wa makabila madogo ambayo yaliogopa utawala wa makabila makubwa, kilijitoa na kujivunja mwaka wa 1964 na wanachama wake wakajiunga na KANU.

Chama kidogo cha upinzani, Kenya People's Union (KPU), kilianzishwa mwaka 1966, kiongozi wake akiwa Jaramogi Oginga Odinga aliyewahi kuwa makamu wa rais Kenyatta. KPU ilipigwa marufuku, na kiongozi kuwekwa kizuizini baada ya chachari za kisiasa zilizohusishwa na ziara za Kenyatta katika Mkoa wa Nyanza. Hakuna vyama vingine vya upinzani vilivyoanzishwa baada ya 1969, kupelekea Kenya kuwa mfumo wa chama kimoja chini ya KANU.

Wakati wa kifo ya Kenyatta (22 Agosti 1978), Makamu wa Rais Daniel Arap Moi, akawa rais wa mpito. Tarehe 14 Oktoba, Moi akawa rais rasmi baada ya kuchaguliwa kama mkuu wa KANU na mteule wake pekee.

Mwezi Juni mwaka wa 1982, bunge lilirekebisha katiba na kufanya rasmi Kenya kuwa nchi ya chama kimoja.

Tarehe 1 Agosti wanachama wa Kenya Air Force walizindua jaribio la mapinduzi, ambalo lilisimamishwa mara moja na vikosi vilivyoongozwa na Jeshi, General Service Unit (GSU) - sehemu ya polisi - na baadaye polisi wa kawaida, lakini si bila ya majeruhi.

Siasa ya vyama vingi[hariri | hariri chanzo]

Baada ya shinikizo kutoka ndani na nje ya nchi, bunge lilifutilia mbali sehemu ya katiba kuhusu chama kimoja mnamo Desemba 1991.

Uchaguzi wa vyama vingi vya kisiasa wa Desemba 1992 ulimpa Rais ushindi chini ya chama cha KANU kwa kupata viti vingi. Rais Moi alichaguliwa tena kwa muda wa miaka mitano, ingawa vyama vya upinzani vilishinda asilimia 45 ya viti vya bunge. Harakati ya demokrasia ya Kenya ilivunjika kabla ya uchaguzi, hivyo basi kuisaidia KANU kubaki madarakani.

Afu zaidi mnamo Novemba 1997 uliruhusu upanuzi wa vyama vya kisiasa kuanzia 11 hadi 26. Rais Moi alishinda upya kama Rais katika uchaguzi wa Desemba 1997, na chama chake cha KANU kilihifadhi viti vingi vya bunge.

Katiba haikumruhusu Rais Moi kukimbilia urais kwa muda mwingine. Moi aliamua kumpa Uhuru Kenyatta fursa ya kugombea urais katika uchaguzi wa Desemba 2002, kwa kumfanya awe mrithi wake. Muungano wa Rainbow wa vyama vya upinzani ulikishinda chama tawala cha KANU, na kiongozi wake, aliyewahi kuwa makamu wa rais Moi, Mwai Kibaki, akachaguliwa kama rais.

Tarehe 17 Aprili 2008, Raila Odinga, kutoka Orange Democratic Movement, mgombea urais katika uchaguzi wa Kenya wa 2007, aliapishwa kama Waziri Mkuu wa Kenya, baada ya miaka zaidi ya arobaini ya kukoma kwa ofisi hiyo.

Angalia Pia[hariri | hariri chanzo]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]