Maumau

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Mau Mau)
Vikosi vya KAR

Maumau lilikuwa kundi la wapiganaji wa Kenya waliokuwa wakipinga utawala wa kikoloni wa Waingereza toka mwaka 1952 hadi 1960.

Kundi lilianzishwa mwaka wa 1946, na viongozi wa hao mashujaa walikuwa Jomo Kenyatta, Jaramogi Oginga Odinga, Paul Ngei, Ronald Ngala, Harry Thuku na wengineo.

Walifanya kazi nzuri sana, kwanza juu ya kuonyesha vile watu wanavyoweza kufika mbali wakiwa kitu kimoja. Kama haingekuwa kwa maungano hawangeweza kufanya chochote.

Ingawa vuguvugu la Maumau halikuwa na mafanikio makubwa kijeshi, upinzani wao ulichangia sana katika kuharakisha upatikanaji wa uhuru wa Kenya mwaka 1963.

Chanzo cha jina la kundi hili, Maumau, hakieleweki vyema. Kuna hali ya kutokukubaliana juu ya chanzo na maana ya jina lenyewe. Baadhi wanadai kuwa ni jina la vilima fulani huko Kenya, wengine wanaamini kuwa jina hilo lilitoka kwa walowezi wa Kiingereza lililokuwa na nia ya kudhalilisha kundi hilo. Wako pia wanaosema kuwa jina hilo ni kifupi cha: Mzungu Aende Ulaya, Mwafrika Apate Uhuru.

Sehemu kubwa ya kundi la Maumau iliundwa na watu wa kabila la Gikuyu huku kukiwa na baadhi ya wanachama toka Embu na Meru. Wagikuyu wenyewe hawakuwa wakiliita kundi hili Maumau bali "Muingi" (vuguvugu), "Muigwithania" (anayeunganisha), "Muma wa Uiguano" (kiapo cha umoja) au KCA (Kenya Central Association, chama kilichotangulia kupigania haki za Wakikuyu.

Makala hii kuhusu mambo ya kihistoria bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Maumau kama enzi zake au matokeo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.