Yohane wa Kety
Yohane wa Kety (kwa Kipolandi Jan z Kęt au Jan Kanty; 23 Juni 1390 - 24 Desemba 1473) alikuwa padri wa Kanisa Katoliki, mwanafalsafa, mwanafizikia na mwanateolojia kutoka Polandi.
Kisha kupewa upadirisho, alifundisha miaka mingi katika Chuo Kikuu cha Krakov. Baada ya kukabidhiwa uchungaji wa parokia ya Olkusz, aliongezea maadili yake ushuhuda wa imani sahihi akawa kwa wasaidizi na wanafunzi wake kielelezo cha ibada na upendo kwa jirani [1].
Papa Klementi X alimtangaza mwenye heri tarehe 28 Machi 1676. Halafu Papa Klementi XIII alimtangaza mtakatifu tarehe 16 Julai 1767[2].
Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 23 Desemba,[3][4] lakini pia 20 Oktoba.
Maisha
[hariri | hariri chanzo]Alizaliwa Kęty, karibu na Oświęcim, Polandi.
Baada ya kusoma chuo kikuu cha Kraków alipopata digrii mbili[5], mwaka 1418 alifikia udaktari wa falsafa.[6]
Miaka 3 iliyofuata alifundisha falsafa na kujiandaa kwa upadrisho.
Baadaye akawa gombera katika shule ya Wakanoni huko Miechow[6], akarudi Krakow kufundisha Sacrae Scripturae (Maandiko Matakatifu). Pia alipata udaktari wa teolojia na kuwa mkuu wa idara hiyo.
Yohane alitumia muda mrefu kunakili vitabu vya Biblia, teolojia n.k.
Katika fizikia, alisaidia kuendeleza theory of impetus ya Jean Buridan, akitangulia michango ya Galileo Galilei na Isaac Newton.
Huko Kraków, alijulikana sana kwa huruma na ukarimu wake kwa maskini, hasa wanafunzi wa chuo kikuu wenye shida. Alijipatia mahitaji halisi tu, ili kugawa mara kwa mara misaada kwa mafukara.
Mara moja alihiji hadi Yerusalemu na mara nne alihiji kwa miguu hadi Roma.[5]
Aliendelea kufundisha hadi kifo chake mwaka 1473, alipokuwa na umri wa miaka 83.
Tazama pia
[hariri | hariri chanzo]- Watakatifu wa Agano la Kale
- Orodha ya Watakatifu Wakristo
- Orodha ya Watakatifu wa Afrika
- Orodha ya Watakatifu Wafransisko
Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]- ↑ https://www.santiebeati.it/dettaglio/30500
- ↑ "Patron Saints Index: "Saint John Cantius"". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2008-10-18. Iliwekwa mnamo 2016-10-23.
- ↑ Calendarium Romanum (Libreria Editrice 1969), p. 111
- ↑ Martyrologium Romanum
- ↑ 5.0 5.1 Godrycz, J. (1910). "St. John Cantius". The Catholic Encyclopedia. New York: Robert Appleton Company.
- ↑ 6.0 6.1 ""St. John Kanty", Catholic Faith Community of Saint John Cantius, St. Cloud, Minnesota". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2016-06-29. Iliwekwa mnamo 2016-10-23.
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- media kuhusu Yohane wa Kety pa Wikimedia Commons
- Biography from the Canons Regular of Saint John Cantius Ilihifadhiwa 26 Oktoba 2016 kwenye Wayback Machine.
- Bull of Canonization (1767) by Pope Clement XIII Ilihifadhiwa 4 Septemba 2012 kwenye Wayback Machine.
- Novena to Saint John Cantius Ilihifadhiwa 26 Oktoba 2016 kwenye Wayback Machine.
- Biography at The Catholic Forum Ilihifadhiwa 3 Januari 2006 kwenye Wayback Machine.
- Patron Saints Index: Saint John Cantius Ilihifadhiwa 18 Oktoba 2008 kwenye Wayback Machine.
- The Saints: A concise Biographical Dictionary, (ed. John Coulson), Hawthorn Books, Inc. 1960 Ilihifadhiwa 19 Aprili 2017 kwenye Wayback Machine.
Makala hii bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari. |